Umaskini, magonjwa na matatizo mengine yanayowakabili binadamu, yamewafanya waamini kila kitu wanachoambiwa na viongozi wao wa dini kama njia ya kuyaondoa.
Muumini akila majani ili kuwa karibu na Mungu
Mchungaji wa nchini Afrika Kusini amewafanya waumini wake wale majani kama mbuzi eti ili waweze kuwa karibu na Mungu.
Mwanamke mmoja alidai kuwa kula majani kulimponya koo lake
Kwa maelekezo ya Pastor Lesego Daniel wa Rabboni Centre Ministries,
mamia ya wafuasi wake walijimwaga kwenye uwanja nje ya kanisa lake kula
majani huko Garankuwa, Kaskazini mwa Pretoria baada ya kuambiwa kuwa kwa
kufanya hivyo wanakuwa karibu na Mungu.
Waumini wakiwa wamelala nje ya kanisa kula majani kama walivyoagizwa na mchungaji wao
Mbinu hiyo yenye utata imekosolewa na watu wengi huku yeye akisema
kuwa binadamu wanaweza kula chochote na wasidhurike. “Ndio tunakula
majani na tunajivunia sababu inaonesha kuwa kwa nguvu ya Mungu, tunaweza
kufanya lolote,” Rosemary Phetha aliliambia gazeti la Afrika Kusini la
Times Live.
Doreen Kgatle, 27, alipata kiharusi miaka miwili iliyopita anasema:
Sikuweza kutembea lakini baada ya kula majani kama mchungaji
alivyoagiza, nilianza kupata nguvu na saa moja baadaye niliweza kutembea
tena.”
Picha zinazoonesha waumini mbalimbali wakila majani huku mchungaji huyu akiwakanyaga zimeleta mjadala mkubwa.
Matokeo baada ya kula majani ni kuumwa tumbo na kutapika
Times Live limeandika kuwa kwenye misa hiyo ya watu takriban 1,000
Daniel alisikika akisema ‘lala’ na watu sita wakalala usingizi.
Aliwaagiza watu wengine kuwapiga vibao na kuwatikisa lakini watu hao
walienda kulala bila kujitambua hadi pale alipowaagiza waamke.
‘Unaweza kuwaacha hivi kwa miezi sita. Naipenda hii. Sipendi kuboreka. Unaweza hata kuwafanya polisi wasinzie pindi wanapokuja kukukamata,” alisema.
>>Bongo5