Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Shaaban Mwamba, juzi usiku alipata kipigo kutoka kwa maofisa wa kikundi cha ulinzi cha chama hicho waliokuwa katika eneo ambalo mkutano wa Kamati Kuu ulifanyika, baada ya kutuhumiwa alikuwa akiwasiliana na wafuasi wa Zitto.
Taarifa kutoka kwa mjumbe mmoja ambaye hakupenda
jina lake litajwe, ilisema kuwa mtu huyo alikuwa akichunguzwa
na maofisa wa ulinzi wa chama hicho muda mrefu, kutokana na nyendo
alizokuwa akizionyesha zilizotia shaka.
Mwandishi wa habari hizi ambaye alikuwa katika
eneo hilo, alishuhudia kiongozi huyo akibebwa juu juu na maofisa hao,
huku akiulizwa aliyekuwa akiwasiliana naye ni nani, kabla ya vijana
wengine wa chama kumkamata na kumweka chini ya ulinzi, wakimtaka atoe
ufafanuzi wa alichokuwa anakifanya.
Baada ya mahojiano ya muda mfupi, kiongozi huyo
alionekana akiinuka na kwenda kunawa kwenye bomba la maji, huku
akitokwa damu mdomoni.
Taarifa zilizopatikana baadaye zilidai kuwa
kiongozi huyo alikuwa akiwasiliana na mama yake Zitto na Katibu wa
Zitto, Dk Alex na kwamba pia simu yake ilikutwa na ujumbe mfupi aliokuwa
amewaandikia watu hao.
Mwandishi wetu alijaribu kumtafuta kiongozi huyo ili
kueleza sababu ya kupigwa kwake, lakini hakupatikana eneo la mkutano
kwa madai kuwa alikwenda hospitali kupata huduma ya kwanza, lakini
hakurudi.
>>Mwananchi
Wakati
hatima ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe ikisubiriwa
kujulikana hapo kesho baada ya Mahakama kutoa hukumu yake, inadaiwa kuwa
baadhi wa wabunge, viongozi na wazee wa Chadema,
wanataka suala hilo liishe mapema.
Habari ambazo zilipatikana jana
zilisema kuwa baadhi ya viongozi hao walitaka Zitto aende Halmashauri
Kuu ya Chadema na kuomba msamaha ili mambo yaishe.
“Walimfuata Kitila (Dk Kitila Mkumbo) wakamwambia
amshawishi Zitto ili mambo yaishe nje ya mahakama, wanataka aende kwenye
Halmashauri Kuu kuomba radhi. Kitila akawaambia kuomba radhi kwa kosa
gani?” kiilisema chanzo hicho.
Hata hivyo, Zitto aliiambia Mwananchi jana kuwa kumekuwa na
jitihada mbalimbali za wazee kutaka kukiepusha chama hicho na migogoro
na kuwa amekuwa tayari kwa suala hilo. “Wazee walikuwa na wajibu wa
kuhakikisha hatufiki hapa tulipofika. Sijui kama fursa hiyo bado ipo,”
alisema Zitto.
Kuhusu uamuzi wake wa kwenda mahakamani alisema:
“Nimekwenda mahakamani kutaka haki itendeke. Chama cha kidemokrasia
kinanyima vipi mwanachama fursa ya kukata rufaa?
“Nisingekwenda mahakamani kama ningeona haki ikitendeka. Tatizo kubwa la chama chetu sasa kinaongozwa na mawazo ya kihuni na yeyote mwenye mawazo ya kujenga anaonekana msaliti.”
“Nisingekwenda mahakamani kama ningeona haki ikitendeka. Tatizo kubwa la chama chetu sasa kinaongozwa na mawazo ya kihuni na yeyote mwenye mawazo ya kujenga anaonekana msaliti.”
>>Mwananchi