Rais Jakaya Kikwete amelihutubia Bunge mjini Dodoma na kueleza kuwa Serikali ya Tanzania haiko tayari kujitoa katika Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.
Rais Kikwete alibainisha kwamba kumekuwa na vikao
visivyo rasmi vinavyofanywa na baadhi ya viongozi wakuu wa Kenya, Uganda
na Rwanda ambavyo vimekuwa vikipitisha mambo yao bila kushirikisha nchi
nyingine ndani ya Jumuiya ambazo ni Tanzania na Burundi.
“Wenzetu wameshafanya vikao vitatu na kupitisha
maamuzi manane ya kushirikiana, kwetu sisi tunadhani hizi ni fujo za
kutaka kuhatarisha uhai wa maisha ya jumuiya yetu ya Afrika Mashariki,"
alisema Rais Kikwete.
Alisema Tanzania itaendelea kuheshimu mambo
yaliyomo kwenye makubaliano ya uanzishwaji wa jumuiya hiyo ambayo ni
umoja wa forodha, soko la pamoja, sarafu ya pamoja na shirikisho la
kisiasa bila kukiuka mlolongo wa utekelezaji wake.
Mbali na suala la Jumuiya ya Afrika Mashariki, pia
Rais Kikwete alizungumzia suala la wanajeshi waliokwenda nchini Congo
DRC kulinda amani, Operesheni Tokomeza dhidi ya ujangili na mchakato wa
Katiba Mpya
Hotuba nzima itawekwa muda si mrefu
Hotuba nzima itawekwa muda si mrefu