Home
»
SIASA
»
ZITTO KABWE KUFUNGA SAFARI YA KWENDA USWISS NA UINGEREZA KUFUATILIA MABILIONI YALIYOFICHWA HUKO
ZITTO KABWE KUFUNGA SAFARI YA KWENDA USWISS NA UINGEREZA KUFUATILIA MABILIONI YALIYOFICHWA HUKO
Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chama Cha Deokrasia na Maendeleo (Chadema) Ndg. Zuberi Zitto Kabwe.
Shirika la Kimataifa la Mtandao wa Ulaya wa Madeni na Maendeleo,
European Network on Debt and Development (Eurodad) watafanya ziara ya
kiuchunguzi kuhusu masuala ya uwazi katika kodi katika nchi za Ulaya
kuanzia tarehe 20 Oktoba mpaka tarehe 5 Novemba mwaka 2013. Uchunguzi
huo utaendeshwa na wataalamu waliobobea wa masuala ya kodi na maendeleo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali wa Bunge la
Tanzania Zitto Zuberi Kabwe ameteuliwa kuongoza Jopo la uchunguzi huo.
Eurodad ni Mtandao wa Mashirika yasiyo ya kiserikali yapatayo 48
kutoka nchi 19 za Ulaya ambayo yanajihusisha na masuala ya kufutia
madeni nchi zilizoendelea, misaada yenye maana na kodi za haki.
Mashirika haya yamekuwa kwenye kampeni ya kupinga utoroshwaji wa fedha
kupitia ukwepaji kodi unaofanywa na mashirika ya kimataifa kwa nchi
zinazoendelea. Zitto amekuwa mmoja wa wabunge wanaosimamia hoja ya
kutaka Watanzania waliotorosha fedha kwenda nje warejeshe na kufunguliwa
mashtaka.Kusoma zaidi.
Mwaka 2012 aliwasilisha hoja binafsi Bungeni na kupitishwa kuwa
Azimio la Bunge ya kutaka uchunguzi kuhusu utoroshwaji wa fedha na
kufichwa nje kama Uswiss. Kikosi Kazi cha Serikali kutekeleza Azimio
hilo la Bunge kinatarajia kuwasilisha taarifa yake katika Mkutano wa
Kumi na Sita wa Bunge. Siku ya Jumatatu tarehe 21 Oktoba Zitto atakutana
na Waziri wa Fedha wa Uswiss na maafisa wa mabenki na asasi zisizo za
kiserikali zilizopo jijini Geneva. Pia Zitto atahudhuria mkutano wa
Kamati ya Kodi ya Umoja wa Mataifa katika kampeni ya kubadili mfumo wa
kodi za kimataifa ili kuzuia unyonyaji wa nchi za Kiafrika unaofanywa na
Makampuni makubwa ya Kimataifa.
Baada ya Geneva Zitto atatembelea nchi za Luxembourg na Brussels
kabla ya kwenda Norway ambapo atamalizia ziara yake kwa Jopo la
Wataalamu wa masuala ya kodi na Maendeleo kuandika taarifa maalumu yenye
mapendekezo kuhusu kuzuia utoroshaji wa fedha kutoka Afrika.
Zitto atakwenda jijini London kutoa mada kuhusu masuala ya kodi za
kimataifa katika mkutano wa Uwazi (Open Government Partnership).
Mwenyekiti wa PAC Tanzania atafanya mazungumzo na Mwenyekiti wa PAC
Uingereza Bi Margaret Eve Hodge, Lady Hodge MBE, PC, MP kuhusu masuala
mbalimbali ya ushirikiano wa mabunge mawili na kuendeleza wito wake kwa
makampuni ya kimataifa kulipa kodi zao barani Afrika na kuacha tabia ya
kutumia ‘Tax Havens’ kukwepa kodi na kufukarisha nchi za Kiafrika