Home
»
MATUKIO
»
YULE MWANAMKE MWENYE UKIMWI ALIYEMCHUKUA MTOTO WA JIRANI NA KUMNYONYESHA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MIWILI JELA
MWANAMKE mmoja raia wa Zimbabwe aliyenyonyesha mtoto
wa jirani bila ruhusa anakabiliwa na kifungo cha karibu miaka miwili
kwa kumwambukiza mtu HIV kwa kukusudia kwa kuwa yeye ni mwathirika.
Annie Mpariwa, 39, alifikishwa mbele
ya mahakama ya Gaborone wiki iliyopita na kesi hiyo iliahirishwa hadi
Oktoba 24 kuruhusu kipimo cha pili cha HIV kufanyiwa mtoto huyo.
Matokeo ya kwanza ya mtoto huyo yalionyesha hana virusi ilhali ya mama huyo yalikuwa na virusi.
Mpariwa alikamatwa wiki jana kwa
mashtaka ya usumbufu na iwapo mtoto huyo atapatikana na virusi, mashtaka
hayo yatazidishwa hadi 'kumwambukiza mtu mwingine HIV kimakusudi.’
Mama
wa mtoto huyo wa miezi 14, Nyasha Mironga, alisema kumwona mwanawe
akinyonyeshwa na jirani wake lilikuwa ni jambo lililomshtua sana.
Kisa hicho kimetokea baada ya
kupitishwa kwa sheria mpya ya HIV/Aids inayotoa adhabu kali zaidi kwa
wale wanaowaambukiza wengine HIV kimakusudi