Sakata la vigogo kuficha mabilioni ya shilingi katika benki za Uswisi, limechukua sura mpya baada ya Serikali ya nchi hiyo kutunga sheria inayowabana walioweka fedha kwenye benki zake kuzithibitisha, la sivyo zitarejeshwa katika nchi husika.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alifanya
mazungumzo na Serikali ya nchi hiyo ambayo imemweleza kuwa imebadili
sheria zake ili kuwadhibiti wageni wanaoficha fedha nchini humo.
Akizungumza na Mwananchi , Zitto alisema amepata
taarifa hizo juzi baada ya kukutana na Waziri wa Fedha wa nchi hiyo
ambaye alimwandalia mazungumzo na watalaamu wake.
Alibainisha kuwa tangu kuibuka kwa sakata hilo
mwaka 2012 na Bunge kuiagiza Serikali kufuatilia, Serikali haijaomba
taarifa yeyote kutoka Uswisi kuhusu Watanzania waliohifadhi fedha nchini
humo.
“Jana nilikutana na Waziri wa Fedha na akatuacha
na mazungumzo na wataalamu wake. Wamesema hadi sasa, Tanzania haijasaini
mkataba wa kubadilishana taarifa za kikodi (Multilateral convention on
administrative assistance in tax matters),” alisema Zitto na kuongeza;
“Kwa kutosaini, Tanzania inajinyima haki ya kupata
taarifa hizi na kutoza kodi kwa watu walioficha fedha huku (Uswisi),
maana Sheria ya Kodi ya Tanzania inataka kila Mtanzania popote anapopata
kipato halali lazima alipe kodi.”
Zitto alieleza kuwa kitendo cha Serikali ya Uswisi
kubadili sheria zake, kinaiwezesha nchi hiyo kutoa taarifa za benki za
watu walioweka fedha nchini humo wakiwamo Watanzania, ambao sasa
watatakiwa kuthibitisha kama fedha hizo ni safi au la.
“Kiufupi, Tanzania haijaomba taarifa yeyote kutoka
Uswisi. Ila Uswisi wamebadili sheria yao na sasa mmiliki wa fedha ndiyo
anapaswa kuthibitisha kwamba ni safi, na ikithibitika kuwa hazina
mwenyewe wala maelezo, zitarudishwa nchi husika,” alisema.
Zitto alisema mbali na kukutana na watendaji hao
wa Serikali amezungumza na Umoja wa Mabenki wa nchi hiyo uliobainisha
kuwa Uswisi ina Watanzania wachache wenye fedha.
“Wamesema Watanzania wengi wana fedha Uingereza,
Jersey, Cayman Islands na Mauritius. Dubai pia imetajwa sana,” alisema
Zitto.
Zitto alielezea kuwa umoja huo wa benki za Uswisi umeanzisha mkakati wa kusafisha fedha uitwao ‘clean money strategy’, na wamegundua watu wengi ambao ni wanasiasa, wamezuia akaunti zao na kupeleka majina kwenye Serikali zao.
Zitto alielezea kuwa umoja huo wa benki za Uswisi umeanzisha mkakati wa kusafisha fedha uitwao ‘clean money strategy’, na wamegundua watu wengi ambao ni wanasiasa, wamezuia akaunti zao na kupeleka majina kwenye Serikali zao.
“Tanzania haijafanya maombi rasmi hapa Uswisi na
hivyo wao kama benki hawawezi tu kutoa taarifa bila kuombwa.
Sheria yao imerekebishwa ambapo sasa ni wajibu wa mwenye akaunti kusema kama fedha zake ni halali au hapana,” alisema Zitto na kuongeza.
Sheria yao imerekebishwa ambapo sasa ni wajibu wa mwenye akaunti kusema kama fedha zake ni halali au hapana,” alisema Zitto na kuongeza.
Hivi sasa hawapokei pesa kutoka nchi za Afrika au
wanapokea kwa tahadhari sana, maana kuna reputational risk (kupoteza
heshima),” alisema.
Werema ahoji...
Ni Bunge?
Hata hivyo, kwa mujibu wa agizo la Bunge, tume hiyo inatakiwa kuwa imekamilisha uchunguzi wake mwezi huu na kuwasilisha ripoti yake katika mkutano huo wa Bunge.
Wito wa timu ya uchunguzi
Zitto alipendekeza timu iliyoundwa kuchunguza
fedha hizo itoe taarifa yake kwenye Mkutano wa Bunge unaoanza Oktoba 29,
mwaka huu, akieleza kuwa, “Kuendelea kukaa na taarifa, kutaongeza
tetesi za kweli au za uwongo.”
Alisema mpango huo wa kusaka fedha zilizofichwa
nchini Uswisi, umelenga zile zilizofichwa na watu binafsi kutokana na
rushwa au kuuza dawa za kulevya na kampuni kubwa za kimataifa.
Alibainisha kuwa wengi waliotambulika ni wanasiasa, vigogo wa jeshi na wakuu wa mashirika ya umma na watendaji wa Serikali.
“Katika mabenki ya Uswisi, kuna kiasi cha Dola za
Marekani 197 milioni. Fedha nyingi zipo katika benki za Uingereza na
visiwa vyake, Dubai na Mauritius,” alisema na kuongeza;
“Wapo watu waliopata fedha kihalali, lakini
wanaficha fedha hizo na mali zao nje ili kukwepa kodi. Wengi wa hao ni
wafanyabiashara wakubwa nchini. Tanzania inapoteza Dola za Marekani 1.25
bilioni kati ya mwaka 2001 na 2012 kwa njia hizi.”
Alibainisha kuwa Tanzania lazima itunge sheria ya kufilisi mali ambazo mtu anashindwa kuthibitisha amezipataje.
“Tayari ninafanyia kazi muswada binafsi wa sheria
wa kubadilisha sheria ya makosa ya jinai ya mwaka 1991.
Wasaidizi wangu wanafanyia kazi muswada huo ili usomwe kwa mara ya kwanza kwenye mkutano wa Bunge unaonza Oktoba 29 na kueleza kuwa sheria ya sasa ina upungufu,” alisema.
Wasaidizi wangu wanafanyia kazi muswada huo ili usomwe kwa mara ya kwanza kwenye mkutano wa Bunge unaonza Oktoba 29 na kueleza kuwa sheria ya sasa ina upungufu,” alisema.
Madai hayo ya Zitto yamekuja ikiwa umepita mwaka
mmoja tangu Bunge kuipa Serikali muda wa kuchunguza sakata la vigogo
walioficha mabilioni katika benki za Uswisi.
Zitto ndiye aliibua sakata hilo mwishoni mwa mwaka
2012. Kufuatia hoja hiyo, Serikali iliunda timu kutokana na Azimio la
Bunge lililotolewa mwishoni mwa mwaka jana.
Werema ahoji...
Ni Bunge?
Timu hiyo inayongozwa na Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, Jaji Frederick Werema ambaye jana baada ya kutafutwa na gazeti
hili alisema, “Uchunguzi kuhusu walioficha fedha Uswisi bado
haujakamilika.”
Viongozi wengine wanaounda tume hiyo ni Mkurugenzi
wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward
Hosea, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Othman Rashid na Gavana wa Benki
Kuu (BoT), Profesa Benno Ndulu.
Alipoulizwa kama kuna uwezekano wa ripoti hiyo
kuwekwa wazi katika Mkutano ujao wa Bunge, Werema alisema, “Kwa nini,
kwani wewe ndiyo Bunge. Uchunguzi bado unaendelea”
Hata hivyo, kwa mujibu wa agizo la Bunge, tume hiyo inatakiwa kuwa imekamilisha uchunguzi wake mwezi huu na kuwasilisha ripoti yake katika mkutano huo wa Bunge.
Alipoulizwa kuhusu ripoti hiyo, Naibu Spika, Job
Ndugai alisema, “Wiki ijayo katika kikao cha Kamati ya Uongozi, Serikali
itatakiwa kutoa taarifa za uchunguzi huo na kama haujakamilika kikao
hicho kitaamua jambo la kufanya na endapo uchunguzi utakuwa umekamilika
zitapangwa taratibu za kuiwasilisha ripoti bungeni.”
Waziri wa Fedha anena
Naye Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa alisema
jana kuwa sheria za kimataifa zipo wazi kwamba fedha chafu
zinazogundulika kufichwa nchi fulani, hurejeshwa katika Serikali ya nchi
husika.
“Lengo la sheria hizi za kimataifa ni kuhakikisha
kuwa fedha za wizi zinazoibwa nchi fulani, haziwezi kuhifadhiwa katika
nchi nyingine,” alisema.
Alipoulizwa kama wizara yake ina taarifa zozote
kuhusu Watanzania walioficha fedha Uswisi alisema, “Kuna Tume iliundwa
na Bunge kufuatilia suala hilo nadhani ndiyo itakuwa na majibu sahihi.”
Uchunguzi wa walioficha mabilioni ya Uswisi
uliibuka baada ya Benki ya Taifa ya Uswiss (SNB) kutoa taarifa mapema
Juni 2012 kuhusu raia wa kigeni wanaomiliki akaunti za benki nchini
humo.
Orodha hiyo inadaiwa kuwa na majina ya baadhi ya
Watanzania wenye akaunti zinazofikia Dola 196 za Marekani milioni ambazo
ni sawa na Sh323.4 bilioni.
-Mwananchi
-Mwananchi