Askari
wa polisi mjini Singida akiwaelekeza washitakiwa wanne wa kesi ya
unyang’anyi wa kutumia silaha kuingia kwenye gari tayari kwenda kuanza
kutumikia adhabu zao kila mmoja miaka 30 jela baada ya kutiwa hatia kwa
kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha.Washitakiwa hao walitiwa hatiani
kwa kosa la kuteka gari la chuo kikuu cha SUA SU 37012 na kisha kuwapora
abiria shilingi 8.7 milioni.Pia walibomoa na kusachi jeneza lililokuwa
limehifadhiwa mwili wa marehemu mwanafunzi wa SUA,Munchari Lyoba
uliokuwa ukipelekwa mkoa wa Mara kwa mazishi.
Mshitakiwa
aliyetiwa hatiani kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha na kupora
abiria wa gari la SUA shilingi 8.7 milioni Hamisi Issah (wa kwanza
kulia) akipanda gari tayari kwenda kuanza kutumikia adhabu yake jela
miaka 30.Pia mwenye kofia ya bakharasia,Abubakari Jumanne naye katiwa
hatiani kwa kosa la unyang’anyi.
Washitakiwa
wanne waliotiwa hatiani kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha
wakiwa kwenye gari la polisi tayari kwenda kuanza adahabu zao za kila
moja miaka 30.Washitakiwa hao walitiwa hatiani kwa kosa la kuteka gari
la chuo kikuu cha SUA na kupora abiria shilingi 8.7 milioni.Washitakiwa
hao pia inadaiwa walibomoa jeneza lililokuwa limebeba mwili wa
mwanafunzi wa SUA Munchari Lyoba na kulisachi kwa imani kuwa limetumika
kuhifadhi mali.(Picha na Nathaniel Limu).
Mahakama
ya wilaya ya Singida imewahukumu vijana wakulima wanne wakazi wa
Manispaa ya Singida adhabu ya kutumikia jumla ya miaka 120 jela baada ya
kupatikana na hatia ya unyang’anyi wa shilingi 8.7 milioni kwa kutumia
silaha.
Washitakiwa hao kabla na baada ya unyang’anyi
huo walitumia silaha aina ya bunduki,nondo,mawe na fimbo katika
kufanikisha azma yao hiyo.
Washitakiwa hao vijana ambao
kila mmoja atatumikia jela miaka 30,ni Hamisi Ally (23),Hamisi Issa
(33),Khalid Hamisi (21) na Abubakari Jumanne (26) wote wakazi wa kijiji
cha Kisaki Manispaa ya Singida.
Mshitakiwa aliyekuwa wa
kwanza kwenye kesi hiyo Idd Omari (38) mkazi wa kijiji cha Kisaki
aliachiwa huru awali baada ya kutokutambuliwa na walalamikaji katika
paredi mbili za utambuzi zilizofanywa na Jeshi la Polisi.
Washitakiwa
hao pia wanadaiwa kuwa baada ya kufanikiwa kupora mali na fedha taslimu
waliweza kubomoa jeneza lililokuwa lina mwili wa mwanafunzi wa SUA,
Munchari Lyoba na kuchana chana sada kwa imani kwamba kuna mali
iliyokuwa imehifadhiwa humo Mwili wa Lyoba alikuwa ukipelekwa Tarime
mkoani Mara kuzikwa.
Kabla ya kutolewa kwa hukumu
hiyo,Mwendesha Mashitaka Sajenti wa Polisi,Godwel Lawrence amesema
pamoja na washitakiwa wote kutokuwa na rekodi yoyote ya makosa ya jinai
lakini kitendo walichokifanya ni cha kinyama na cha aibu mbele ya macho
ya jamii.
“Kwa hiyo,Mheshimiwa hakimu naiomba mahakama
yako tukufu iwape washitakiwa wote adhabu kali ambayo itakuwa fundisho
kwao na watu wengine wanaotarajiwa kufanya makosa ya jinai kwa kutumia
silaha au nguvu ya aina yoyote”,amesema Lawrence.
Kwa
upande wao washitakiwa kila mmoja kwa nafasi yake walitoa maombolezo
yaliyofafana kwamba wana familia zinazowatengea kwa asilimia kubwa na
kwamba kosa hilo ni la kwanza kutenda toka wazaliwe Hivyo wakaiomba
mahakama hiyo iwape adhabu nafuu.
Akisoma hukumu hiyo
iliyochukua saa moja na dakika 45,Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya
ya Singida,Flora Ndale amesema usahidi wa upande wa mashitaka
umethibitisha bila kuacha chembe chembe ya shaka kwamba washitakiwa wana
hatia kama walivyoshitakiwa.
“Walalamikaji wote ambao
walikuwa abiria kwenye gari lililokuwa likisafirisaha mwili wa marehemu
mwanafunzi wa SUA maelezo yao yanafafana wote waliweza kuwatambua vema
washitakiwa kwa msaada wa taa za gari na mbalamwezi”,amesema.
Ndale
amesema kiongozi wa msafara huo Makaranga Nona,aliiambia mahakama
kwamba mshitakiwa wa pili na wa tatu walimwamuru kufungua ‘brief case’
mbele ya gari huku mwanga wa taa za gari ukiwamulika.
“Kama
hiyo haitoshi,dereva wa gari hilo Kalistus Malipula ameiambia mahakama
hii kwamba mshitakiwa wane alimbebeleza kwa muda mrefu ampe simu mbili
za marehemu na maombi hayo alikuwa akiyatoa huku mwanga wa taa za gari
ukimmulika”.
Kwa mujibu wa Mwendesha Mashitaka Lawrence
washitakiwa hao wametenda kosa hilo Desemba sita mwaka jana saa saba
usiku huko katika barabara kuu ya Dodoma – Singida eneo la kijiji cha
Kisaki.
CREDIT : MO DEWJI