mwanamke
huyu akiwa amepewa msaada na wasamaria wema ili kumwahisha hospitali
UMASIKINI nijanga lisilo kubalika katika jamii yoyote.
TANZANIA ikitajwa kuwa ni miongoni mwa nchi zenye amani na utulivu, imebainika kuwa Watanz ania ni miongoni mwa watu wasio na furaha na waliokata tamaa hapa duniani.
TANZANIA ikitajwa kuwa ni miongoni mwa nchi zenye amani na utulivu, imebainika kuwa Watanz ania ni miongoni mwa watu wasio na furaha na waliokata tamaa hapa duniani.
Ripoti
inayoonyesha orodha ya nchi zenye furaha duniani ya mwaka 2013 (World
Happiness Report 2013), imeitaja Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi 10
za mwisho duniani kati ya nchi 156 zilizofanyiwa utafiti huo.President Jakaya Kikwete.
Ripoti
hiyo iliyoandaliwa na kundi la wataalamu kutoka Umoja wa Mataifa (UN),
kati ya mwaka 2010 na 2012, inaonyesha kuwa Tanzania imeshika nafasi ya
151 ikiburuta mkia pamoja na nchi za Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Afrika
ya Kati, Benin na Togo.
Upatikanaji
wa huduma za jamii, mtazamo wa watu kuhusu rushwa, umri wa kuishi,
ukosefu wa kazi, pato la taifa na ukarimu wa watu katika nchi husika, ni
baadhi ya vigezo vilivyoangaliwa wakati wa kuandaa taarifa hiyo.
Waziri
wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka alieleza kushtushwa na ripoti hiyo
kwa maelezo kwamba ni asilimia 11.7 tu ya Watanzania wasio na ajira na
kwamba wale wanaofanya kazi, wanapata huduma zote za msingi, ikiwa ni
pamoja na kwenda likizo na mishahara inayolingana na taaluma zao.ZAHANATI
zinahitajika vijijini nchini tanzania kote zinawe jutoa huduma bora
wauguzi wakutosha maabara bora na zenye vifaa vya kisasa magari ya
wagonjwa LAKINI NCHINI TANZANIA usishangae viongozi kujipongeza
kwakupata nyadhifa wakiishi maisha ya kifahari huku watu wakifa
kwakukosa dawa mahospitalini wajawazito wakifia njiani kutokana na ubali
wa kituo cha afya shule zikiwa hazina vyooo walimu hawapo wakutosha
majengo mabovu madawati hakuna vitabu hakuna na kila kanda na mtaala
wake AMAKWELI KUFA KUFAANA TANZANIA viongozi matajiri wananchi masikini
wakutisha UMASIKINI WA TANZANIA janga la kupandikizwa NITAUCHUKIA
UMASIKINI NA KUUPIGA VITA HADI TONE LA MWISHO LA DAMU YANGU nakataa
umasikini ujinga na maradhi sio haki ya watanzania
“Watanzania
wana furaha, kwa upande wa wafanyakazi wanapata haki zao zote
wanazostahili, sijui ni vigezo vipi wametumia…kwa mujibu wa takwimu za
2006 ni asilimia 11.7 ya Watanzania ndio waliokuwa hawana kazi, lakini
wakati huo idadi ya watu ilikuwa ndogo, hivi sasa imeongezeka,” alisema
Kabaka na kuongeza:“Usafiri ndiyo tatizo linalowasumbua wafanyakazi
wengi kwa kuwa wanachelewa kwenda kazini.”
Naye,
Naibu Waziri wa Fedha, Saada Salum alisema pamoja na vigezo vingine
vilivyotumika kutambua furaha ya Watanzania, umaskini ndiyo unaoweza
kuwa chanzo cha Tanzania kushika nafasi za mwisho.
“Inategemea
na vigezo vingine walivyovitumia, nakubali kuwa Tanzania ni maskini
pengine hali hiyo imeifanya nchi kushika nafasi ya mwisho,” alisema
Salum.
Nchi zilizoongoza
Taarifa
hiyo imezitaja nchi tano; Denmark, Norway, Uswisi, Netherlands na
Sweden kuwa ndizo zinazoongoza kwa watu wake kuwa na furaha zaidi
duniani, huku Angola ikishika nafasi ya kwanza Afrika na ya 61 duniani
ikifuatiwa na Algeria (73), Libya (78), Ghana (86), Zambia (91), Lesotho
(98), Morocco (99) na Swaziland (100).
Kwa
upande wa Afrika Mashariki, wananchi wa Uganda ndio walionekana kuwa na
furaha zaidi kwani nchi hiyo imeshika nafasi ya 120 wakifuatiwa na
Kenya (123), Tanzania (151), Rwanda (152) na Burundi (153).
Ripoti
hiyo inabainisha kuwa kati ya mwaka 2005 na 2012, nchi 60 duniani
ziliongeza viwango vya furaha kwa watu wake, kati ya hizo 16 zikiwa
barani Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara.