Msafara
wa rais Jakaya Kikwete ukiwa umesimama kwa muda eneo la msitu wa
taifa wa Sao Hill Mufindi katika barabara kuu ya Iringa- Mbeya
kufuatia moto mkubwa kuwaka katika msitu huo mchana wa leo
Askari
polisi akisimamisha msafara wa rais Kikwete kutokana na moto mkubwa
kutanda eneo hilo la Changalawe katika msitu wa Taifa wa Sao Hill
umbali wa mita mbili kuelekea barabara ya Ikulu ndogo mjini Mafinga
Askari
wa FFU wakishuka katika gari lao kwenda kuangalia usalama wa rais
Kikwete na kulia gari la kwanza ni naibu waziri wa ujenzi gari la pili
la la tatu ni magari ya Ikulu yakiwa yamesimama
hapa
askari wakishuka kuingia katika moshi mzito kuangalia usalama wa
rais katika eneo hilo ambalo moshi mzito ulitanda barabarani
Msafara ukipita eneo hilo salama huku kulia ni askari wa JKT mafinga wakizima moto huo
YAKIWA
ni masaa takribani mawili kupita kutoka Rais Jakaya Kikwete kufanya
kikao chake cha majumuisho ya ziara yake na viongozi wa mkoa wa
Njombe na kuwataka kuchukua hatua katika kuthibiti moto ili
kuepusha ukame ,moto mkubwa umezuka katika msitu wa Taifa wa Sao Hill
Mufindi na kupelekea msafara wa Rais kusimama kwa muda kiusalama
kutoka na moshi mzito uliotanda barabara kuu ya Iringa Mbeya .
Moto
ulio ulioanza kuwaka mida ya saa nane mchana ulizuia kwa muda
kama dakika tatu hivi msafara wa Rais Kikwete kufimama katika eneo la
Changalawe mjini Mafinga umbali wa mita 2 kufika njiapanda ya
kuingia ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mufindi na Ikulu ndogo ya wilaya
ya Mufindi.
Kutokana
na tukio hilo la moto msafara wa rais Kikwete ulisimama na baada ya
maofisa usalama kushuka na kutazama usalama zaidi wa msafara huo
ndipo walioruhusu msafara huo kuendelea .
Hata
hivyo jitihada kubwa zilionekana kufanywa na kikosi cha askari
wa JKT Mafinga pamoja na wananchi ambao walikuwa wakizima moto
huo .
Huku
vyombo vya usafiri yakiwemo mabasi ya abiri yanayosafiri kutoka Dar
es Salaam kuwenda mikoa ya kusini na nchi za kusini mwa Tanzania
yakikwama kuendelea na safari kutoka na moto huo kushikakasi na
moshi mzito kutanda barabara
Mkuu
wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma alisema kuwa uongozi
wa mkoa tayari umeagiza mkuu wa wilaya ya Mufindi kuwasaka
waliohusika na uchomaji moto huo ili kuchukulia hatua kali.
Mkuu
huyo wa mkoa alisema kuwa mkoa wa Iringa umekuwa ukichukua hatua
kali kwa wale wote wanaoanzisha moto kichaa kama huo hivyo kupitia
ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mufindi wahusika watasakwa popote walipo .
Mbali
na hilo mkuu huyo amelipongeza jeshi la JTK Mafinga kwa kuchukua
hatua za haraka katika kukabiliana na moto huo huku akisema madhara
zaidi yatokanayo na moto huo yatatolewa baada ya moto huo
kuthibitiwa