Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa
Mkapa aliyasema hayo mjini hapa katika mahafari ya kwanza ya Chuo kikuu
cha Askofu Mihayo Tabora (AMUCTA ), chuo kishiriki cha mtakatifu
Agostino yalifanyika kwenye viwanja vya chuo hicho mjini Tabora.
Alisema kuwa anahisi jamii kwa sasa ina ari ya kutafuta majibu ya
matatizo na changamoto zinazowakabili na kutokana na njaa kubwa ya
maendeleo inapendelea kudakia kupata majibu ya haraka haraka kama vile
matangazo ya biashara katika radio na runinga, badala ya kuwa tayari
kuonesha utayari wa kutumiza wajibu.
Alisema matokeo yake ni malalamiko yasiyoisha na kusahau kwamba subira
yavuta heri, na kuongeza kuwa kiini cha matatizo kinapaswa kichunguzwe
kwa makini na changamoto ya elimu inavyoweza kukabiliwa.
Alisema kwa njia hiyo wigo wa fikra utapanuliwa na kuweka misingi imara
zaidi ya kutatua matatizo yanayozunguka jamii hasa elimu na miundombinu
mbalimbali.
Awali mkuu wa chuo cha AMUCTA, Padre Dk. Javenalis Asantemungu, alisema
chuo hicho, kilianza rasmi Novemba 2010 kikiwa na wanafunzi 885, ambapo
51 waliahilisha masomo kutokana na sababu mbalimbali wawili walifariki
dunia, 116 wamesoma hadi mwisho lakini hawakutimiza vigezo vya kuhitimu.
Wahitimu wa jana walikuwa 718.
Padre Asantemungui aliwataka wakazi wa mkoa wa Tabora ambao hawawezi
kujiunga na masomo ya asubuhi na mchana chuo kinaendesha mafunzo ya
shahada ya Uzamili kwa muda wa jioni, utaratibu huo umeanza kuitikiwa na
watumishi mbalimbali wa serikali na sekta binafsi.
SOURCE: NIPASHE JUMAPILI