Mkurugenzi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw.Charles Magaya akiongea kuhusu maadhimisho ya Mwalimu Nyerere wakati wa kikao kazi kilichofanyika mjini Dodoma mapema leo.Kulia kwake ni Mkurugenzi Msaidizi Bw.Athanas Kolokota na Mkurugenzi Msaidizi Thomas Manyambula (kushoto).
Na Happiness Shayo-Utumishi
Maadhimisho ya kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere yanatarajiwa kufanyika kitaifa kesho katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.
Hayo
yalisewa na Mkurugenzi Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa,Ofisi ya
Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw.Charles Magaya alipokuwa katika
kikao kazi cha maandalizi ya siku hiyo mjini Dodoma.
Bw.Magaya alisema Siku ya kumuenzi Baba wa Taifa itaongozwa na mmoja wa washiriki wa Baba wa Taifa Balozi Job Lusinde.
“Maadhimisho
hayo yataongozwa na mmoja wa washiriki wa Baba wa Taifa katika
kupigania Uhuru wa Tanganyika Mheshimiwa Balozi Lusinde ambaye pia ni
muasisi wa Chama cha TANU”alisema Bw.Magaya.
Sambamba
na maadhimisho hayo Bw.Magaya alisema kuwa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya
Utumishi wa Umma imeandaa sinema mbalimbali za Mwalimu Nyerere
zitakazoonyeshwa katika viwanja vya Nyerere Square leo kuanzia saa 12
jioni hadi saa 3 usiku.
Aidha,aliwataka wananchi wa mkoa wa Dodoma kushiriki katika maadhimisho hayo ya kumuenzi Baba wa Taifa.
Pia
Bw.Magaya alitoa wito kwa viongozi wa Mkoa wa Dodoma kuhamasisha
wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye viwanja vya Nyerere Square ili
kusikiliza hotuba mbalimbali kutoka kwa viongozi waliofanya kazi karibu
na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.
Maadhimisho
ya Baba wa Taifa hufanyika Oktoba 14 ya kila mwaka ambapo mada
mbalimbali hutolewa na viongozi waasisi wa Taifa la Tanzania.