Daladala aina ya Coster yenye namba za
usajiri T.960 AQY inayofanya safari zake za Kibwabwa mjini Iringa mara
baada ya kugongana na gari aina ya Isuzu Tipa, lenye namba SM 3363
katika Mlima wa Ipogolo eneo la Kisima cha Bibi.
Taxi ambayo nayo ilisababishiwa ajari
ikiwa katika eneo la tukio, huku askari polisi wakilinda usalama wa mali
za abiria na baadhi ya vitu katika eneo la tukio.(A.M)
Wananchi wa mji wa Iringa wakitazama ajari hiyo katika mlima wa Ipogolo (Kisima cha Bibi).
Basi aina ya Coster linalofanya ruti zake
Kibwabwa Manispaa ya Iringa likiwa eneo la tukio, baada ya kugongana na
Roli Tipper na kusababisha ajali iliyojeruhi zaidi ya watu 30.
ZAIDI ya abiria 38 wamejeruhiwa katika
ajali iliyohusisha magari manne mjini Iringa, baada ya Bus dogo la
abiria aina ya Coster kufeli breki na kuyagonga magari matatu, ajali
ambayo imetokea majira ya saa saba mchana wa siku ya jana.
Tukio hilo limetokea katika mlima wa
Ipogolo, eneo maarufu mjini Iringa kama "Kisima cha bibi", ambapo ajali
hiyo imesababisha majeruhi 38 ambao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa
mkoani Iringa, huku chanzo cha ajali hiyo kikisemekana kuwa na kuferi
breki kwa Bus hilo la abiria,lenye namba T. 960 AQY na kuyavaa magari
matatu, gari kubwa aina ya Tipper Isuzu SM784 BNA la manispaa ya Iringa,
Tax pamoja na Hiace.
Akizungumzia hali ya majeruhi wa tukio
hilo , Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa Dr.
Deogratius Manyama amesema wamepokea majeruhi 38, na waliolazwa ni 8
huku majeruhi watatu wakiwa na hali mbaya, na kuwa majeruhi wengi
wameumia zaidi kichwani na kifuani, huku majeruhi 27 wakiruhusiwa kurudi
nyumba kwao kutokana na kutokuwa na majeraha makubwa.