Jeshi la polisi wilayani Makete mkoa wa Njombe linamshikilia Bi Rose Skwea Tweve mkazi wa kijiji cha Isapulano kwa tuhuma za kummwagia maji ya moto mke mwenzake Estina Kristian Sanga [23] pamoja na mtoto wake mdogo ambao wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Makete kwa matibabu zaidi.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo mratibu wa polisi ambaye pia ni afisa upelelezi
(OCCID) wilaya ya makete Gosbert Komba amesema matukio ya kujichukulia
sheria mkononi yamekuwa yakijirudia mara kwa mara wilayani hapo huku
akiwataka wananchi kufuata sheria na taratibu za nchi.
Kwa upande
wake Bi Estina Sanga Ambaye amejeruhiwa na mke mwezake huyo amesema kuwa
tukio hilo lilimpata majira ya saa mbili usiku alipokuwa anakwenda
kumjulia hali mume ambae ni mgonjwa nyumbani kwa Bi Rose ambaye ni Bi
mkubwa.
Naye mtuhumiwa wa tukio hilo Bi Rose Tweve amesema
alifikia hatua hiyo baada ya kurushiana maneno na mke mwezie huyo na
kuchukizwa kwa kitendo cha kwenda kumuona mume wao huku akiwa amelewa
ndipo akachua sheria mkononi kwa kumwangia maji ya moto kama njia ya
kumuonya.
Akizungumzia tukio hilo Bwana Itiso Chaula (32) ambaye ni
mume wa wanawake hao mkazi wa kijiji cha Isapulano amesema ameshangazwa
na tukio ambalo Bi mkubwa amelifanya kwa Bi mdogo na kulaani kitendo
hicho.
Occid Komba amesema mtuhumiwa huyo anashikiliwa na polisi huku upelelezi ukiendelea, lakini amesema kwa taarifa alizonazo majeruhi anaendelea na matibabu baada ya kujeruhiwa na maji moto usoni na maeneo ya kifuani
NA EDWIN MOSHI, GLOBU YA JAMII MAKETE