BIBI Mariam Mponzi (80) amepambana kwa hali na mali kuwatetea wajukuu zake waliotelekezwa na baba yao Emmanuel Yuta.
Emmanuel alidaiwa kuuza nyumba waliyokuwa wakiishi katika Kijiji cha Hatwelo, Kata ya Ijombe, Mbeya Vijijini na kutokomea kusikojulikana huku akiwaacha watoto wake wawili wenye umri wa miaka 9 na 11 wakikosa pa kuishi.

Kikongwe huyo
alichukua hatua hiyo baada ya kubaini kuwa kitendo kilichofanywa na
mwanaye kwa kushirikiana na serikali ya kijiji si cha kiungwana.
Bibi huyo
alilazimika kukopa shilingi laki nne kutoka kwa mtu ambaye hakumtaja
jina kwa lengo la kuzirejesha kwa mtu aliyenunua nyumba hiyo aitwaye
Dati Nsagaje ambaye alisema akirudishiwa fedha zake angeiachia nyumba
hiyo.
Akizungumza
baada ya kurejeshewa nyumba hiyo, kikongwe huyo alisema kwa sasa makazi
hayo ni mali ya wajukuu zake hivyo mwanae akishindwa kuendelea na maisha
huko alikokimbilia na kuamua kurejea akatafute sehemu nyingine ya
kuishi.
Baadhi ya majirani wa eneo hilo walisema kitendo alichokifanya baba wa watoto hao hakipaswi kufumbiwa macho na mlalamikiwa akikamatwa achukuliwe hatua kali za kisheria
Baadhi ya majirani wa eneo hilo walisema kitendo alichokifanya baba wa watoto hao hakipaswi kufumbiwa macho na mlalamikiwa akikamatwa achukuliwe hatua kali za kisheria