Hali
si shwari katika klabu ya wasanii wa filamu za Kibongo, Bongo Movie
Unity ikidaiwa kuwa baadhi ya ‘memba’ wake wanashinikiza mwenyekiti
wake, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ajiuzulu.
Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
Habari
zilizoifikia Stori Extra wikiendi iliyopita zilidai kuwa, baadhi ya
wasanii wa klabu hiyo akiwemo mwenyekiti huyo walilamba mshiko kutoka
kwa mwanasiasa mmoja wa CCM mkoani Mbeya ili wamfanyie kampeni katika
uchaguzi ujao jambo ambalo wenzao walilipinga vikali kwa kuwa wao
hawajihusishi na siasa bali wasanii na jamii.
Alipotafutwa Steve kujibu tuhuma hizo hakupatikana lakini katibu wake, William Mtitu alikiri kuwepo kwa ishu hiyo.