Rubani msaidizi wa ndege ya Ethiopian Airlines iliyokuwa ikienda Roma toka Addis Ababa ameteka ndege hiyo mapema leo na kuilazimisha itue Geneva, Uswisi, polisi wameieleza AFP.
Rubabi huyo alitenda kitendo hicho cha ajabu kama
njia ya kujaribu kuomba hifadhi ya kisiasa nchini Uswisi. “Anadai
anaishi kwa hofu nchini kwake mwenyewe, hivyo anataka hifadhi Uswisi,”
vyanzo vya kipolisi vimeiambia AFP.
Tukio lilivyotokea
Wanausalama Geneva wanasema rubani huyo msaidizi
alivizia mwenzake alipokuwa amekwenda kujisaidia, kisha akajifungia
katika chumba maalum cha kuongoza ndege na kubadili uelekeo wa chombo
hicho kukipeleka Uswisi.
Baada ya hapo, kijana huyo mwenye umri wa miaka 31
ambaye ni raia wa Ethiopia aliomba idhini ya kutua Geneva akidai
anahitaji mafuta ya dharura. “Ghafla, akatutangazia kuwa ameteka ndege,”
vimesema vyanzo hivyo.
Safari zasimama, huduma zavurugika
Kutokana na hati hati hiyo, ilibidi safari zote
kuingia na kutoka uwanjani hapo zisitishwe mapema leo. Hata hivyo,
kufikia saa 2:45 asubuhi kwa saa za ulaya ya kati, hali ya utulivu
ilishaanza kurejea.
Polisi wamemtia ndani mteka ndege huyo, ambaye
anatarajiwa kufikishwa mahakamani Jumatatu ijayo, zasema taarifa
zilizoifikia AF