MWALIMU wa Shule ya Msingi Mwang’osha Kata ya Nyamalongo wilayani Shinyanga, Christipian Mafuru (24) amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa madai ya msongo wa mawazo.
Mafuru
ambaye alitumia kamba ya katani na kujinyonga kwenye choo chake.
Ameacha ujumbe uliosomeka ‘Msongo wa mawazo umenilazimu nifanye hivi,
poleni sana walimu wenzangu, samahani wazazi wangu, kwa heri mwanangu
Ray.’
Mwalimu
Mkuu wa Shule hiyo, Frida Maleko aliwaeleza waandishi wa habari kuwa
waligundua mwili wake juzi saa 9:30 alasiri baada ya kutoonekana shuleni
kwa muda mrefu.
Kwa
mujibu wa Mwalimu Maleko, aliamua kumpigia Mwalimu Mafuru (marehemu)
simu bila kupatikana na ndipo aliamua kwenda na walimu wenzake nyumbani,
ambako mlango ulikuwa umefungwa huku simu ikiita.
Alisema
hali hiyo iliwatia shaka, hivyo kuamua kuvunja dirisha la nyumba hiyo,
ambako hawakukuta mtu, isipokuwa ujumbe huo ulioandikwa na kuachwa
mezani. Mwalimu huyo aliajiriwa mwaka jana katika shule hiyo na alikuwa
mchapakazi.
“Nilishituka
kwa kutomwona muda mrefu shuleni, ikabidi nimpigie simu nimuulize
kulikoni hujafika shule leo, lakini simu haikupokewa,”alisema Mwalimu
Mkuu.
Baada ya kutomwona ndani, baadaye waligundua mwili wake ukiwa chooni.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Evarist Mangalla alithibitisha tukio
hilo na kwamba chanzo cha kifo ni msongo wa mawazo na hiyo inatokana na
ujumbe alioandika kwa mkono wake na kutia saini.
Alisisitiza hakuna mtu anayeshikiliwa na Polisi juu ya kifo hich