“It was a surprise,” Jokate ameiambia Bongo5. “Alinialika two weeks ago lakini sikuwa na uhakika kama ntaweza kwenda kutokana na ratiba zangu lakini later on nikasema ngoja nisimjibu, sikuongea naye tena kitu chochote. Kwahiyo nikaamua mimi na rafiki zangu kwenda Arusha, nikaamua tu
kumsuprise. Hakujua kama tupo wala sikusema popote kwamba naenda,”ameongeza Jokate.
Wema na Jokate wakiwa kwenye show ya Mirror jijini Arusha
“It was crazy,” amesema Jokate kuelezea ilivyokuwa baada ya yeye kupanda jukwaani. “It was nice though, kila mtu aliappreaciate, nadhani hicho ndio kitu kilichokuwa muhimu. I was also a bit nervous, sijawahi kufanya kitu kama kile na sikujua watu wataipokeaje but it was great. Kila mtu alifurahi, nadhani tumeipa pia heshima show yake.”
Wema na Jokate wakicheza muziki pamoja
Jokate amesema yeye na Wema walikuwa wameshaziweka tofauti zao muda mrefu kuanzia kipindi kile kwenye msiba wa baba yake Wema, mwishoni mwa mwaka jana.
“Kwasababu ulikuwa msiba sikuweza kuweka public kwasababu msiba ni kitu sensitive sio vizuri kuchukua advantage kufanya vitu vingine ambavyo havieleweki. Naweza kusema ile ndio ilikuwa public appearance ya kwanza,” amesema Jokate.
Jokate amesema hakuna tena tofauti kati yake na Wema na siku za usoni wanaweza kushirikiana katika mambo mengi ya kazi.
“I like it cause kuna wasichana wengi they look up to us. Tuangalie zaidi kushirikiana kuliko kuwa na vitu ambavyo havieleweki na havina mtazamo mzuri kwenye jamii. Na mimi hasa hicho ndio kilinisukuma kwamba do something kwenye event yake, kuonesha tu kwamba tunaweza kushirikiana na kufanya vitu positive kwenye jamii.”
Msikilize zaidi hapo chini.