MREMBO
mmoja ambaye alihu-dumu kwenye nyumba ya kulala wageni na baa (jina
tunalo) iliyopo Tengeru, wilayani Arumeru, mkoani Arusha, Blandina
Michael (33) amekutwa amekufa kwenye moja ya vyumba vya nyumba hiyo huku
chanzo cha tukio hilo kikihusishwa na vitendo vya ushirikiana.
Taarifa
za awali zilimtuhumu mmiliki wa nyumba ya wageni moja ambaye pia
anajihusisha na biashara za madini (jina tunalo) kwamba alimtoa kafara
mhudumu huyo. Ilidaiwa kuwa, kila mwaka mtu mmoja katika biashara zake
hupoteza maisha ghafla.
Hata
hivyo, mfanyabiashara huyo alipoongea na Uwazi juzikati alikanusha
vikali tuhuma hizo na kueleza kuwa yeye ni muumini mzuri wa imani yake.
‘’Hao
watu wanapotosha sana, unajua kuna mwaka mwanaume mmoja alikufa ghafla
kwenye nyumba yangu ya kulala wageni, alikuja na mpenzi wake ila alimeza
Viagra ambazo hata polisi walizikuta mezani.
“Sasa watu wasio na nia njema na mimi tukio hilo wanaliunganisha na hili kwamba nawatoa kafara,” alisema.
“Sasa watu wasio na nia njema na mimi tukio hilo wanaliunganisha na hili kwamba nawatoa kafara,” alisema.
Kifo
cha Blandina kilitokea ndani ya chumba huku mtu mmoja anayedaiwa kuwa
mpenzi wake aliyejulikana kwa jina moja la Timo, mkazi wa eneo hilo
akihojiwa na polisi.
Marehemu
Blandina ambaye ni mzaliwa wa mkoa wa Tanga, anaelezwa na bosi wake
huyo kwamba alikuwa kama mtoto wa familia yake kwa vile alimwamini sana.
Alifanya kazi hapo kwa miaka 8 na hakuwa na tatilo la kiafya.
Bosi
huyo alisema mwili wa marehemu uligundulika baada ya mfanyakazi
mwenzake wa kiume kumpigia simu saa 2 asubuhi ambapo simu yake ilikuwa
ikiita bila kupokelewa ndipo alipoamua kwenda kumgongea katika chumba
hicho.
Alisema
baada ya kufika alishangaa kukuta mlango wa chumba chake uko wazi na
alipochungulia alibaini kwamba Blandina alikuwa amefariki dunia.
Hata
hivyo, polisi baada ya kufika na kuufanyia uchunguzi wa awali mwili huo
hawakugundua kuwepo kwa jeraha lolote linaloashiria kuuawa, ingawa
mwili huo ulipelekwa kufanyiwa uchunguzi wa kitaalam katika Hospitali ya
Mkoa ya Mount Meru.
Jeshi
la Polisi mkoani Arusha limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema
kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti
katika hospitali hiyo.