Ujira wa usaliti ni aibu kubwa! Mwanaume aliyefahamika kwa jina la
Baba Anorld almaarufu Ngosha, amedai kumfumania laivu mkewe, Anjela
‘Mama Anorld’ akiwa chumbani na shemeji yake aliyetajwa kwa jina moja la
Paulo.
Fumanizi hilo lilitokea usiku wa kuamkia Jumatano wiki hii, nyumbani
kwa wanandoa hao huko Vingunguti-Mikoroshoni, Dar baada ya Ngosha
kumwekea mkewe huyo mtego.
Ilielezwa kuwa awali, Ngosha alikuwa akishirikiana na Paulo kwa mambo
mengi na hakuwa na shaka naye lakini kuna siku moja majirani
walimwambia ‘Oyaaa…babu shtuka mali zako zinaliwa, tena kikulacho ki
nguoni mwako’.
Ilielezwa kuwa baada ya kuambiwa maneno hayo alitafakari lakini
akashindwa kupata majibu hadi pale alipotamkiwa kabisa kuwa jamaa yake
anamsaliti kwa mkewe.
Ngosha alisema katika uchunguzi wake, wapambe walimng’ata sikio kuwa
anazungukwa na Paulo ambaye amekuwa akimuita mama Anord shemeji huku
akimng’ong’a Ngosha kisogoni.
Ilisemekana kuwa wapambe hao walimtonya Ngosha kuwa akiwa hayupo mgoni huyo na mkewe huingia chumbani kwake na kufanya yao.
MTEGO WATEGWA, OFM MZIGONI
Habari zilieleza kuwa baada ya ‘kujazwa sumu’ juu ya taarifa hizo, Ngosha aliwaomba wapambe hao wamsaidie kutega mtego huku Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers ikiomba kuingia mzigoni.

ILIKUWAJE?
Ngosha aliambiwa ajifanye amesafiri na kutarajia kurudi kesho yake.
Akiwa kazini, alimpigia simu mkewe akamtaarifu kwamba asimuandalie chakula kwa kuwa kuna ‘kijisafari’ cha dharura na kutarajia kurudi kesho yake.

Ngosha hakusafiri, badala yake alikuwa mtaa wa pili huku mashushushu
wake wakilizunguka eneo la tukio na kuangalia kila kilichokuwa
kikiendelea kisha kutoa taarifa kwake.
PAULO AWASILI KWA MBWEMBWE
Ilipofika saa 3:43 usiku, Paulo aliwasili eneo la tukio na kuingia chumbani kwa Ngosha akiwa na kifurushi chenye chipsi na vipapatio vya kuku.

Bila kujua nje kuna wapigachabo waliopandikizwa na Ngosha, wawili hao
walianza kupiga stori za ‘Kivalentine’s Day’ wakijua mwenye ndoa yake
alikuwa safarini.
‘TAP’ TAA YAZIMWA
Kwa mujibu wa wapigachabo hao, saa 6:12 usiku, yale mazungumzo yalikatika ambapo wawili hao walizima taa ndipo mashushushu walipomtaarifu Ngosha.

NGOSHA ARUKIA MLANGO
Saa 6:14 usiku, Ngosha alipokea simu kutoka kwa wapigachabo wake waliomtaarifu kuwa tayari mambo ‘yamekwiva’ chumbani kwake na ndipo mwenye mali huyo alipokimbilia eno la tukio.
Alipofika aliurukia ‘samasoti’ mlango wa mninga ambao ulimdindia na kukataa kuvunjika.

Ngosha, akiwa kwenye tafakuri kuntu ya namna ya kuvunja mlango, baba
mwenye nyumba aliyejitambulisha kwa jina moja la Ndosi alitokea na
kumdhibiti huku akimsihi asifanye vurugu wala kuua mtu bali ajaribu
kuwagongea kiustaarabu ili kuunusuru mlango wake.
WAVAA CHAPUCHAPU
Saa 6:21 usiku, wakati wakigongewa walitumia nafasi hiyo kuvaa chapuchapu na kufungua mlango wenyewe ambapo liliibuka varangati zito kati ya wawili hao walionaswa na Ngosha na kundi lake ambapo palichimbika.

Kitendo cha kumfumania mkewe laivu kilimfanya Ngosha amwage chozi la kiutu umzima kutokana na kutoamini alichokishuhudia.
MGONI APIGWA FAINI
Saa 6:45 usiku, ingawa varangati lilikuwa kubwa lakini wasamaria wema waliingilia kati na kuwatuliza kisha kuwataka Ngosha na mgoni wake (Paulo) wakae kitako na kuyazungumza kiutu uzima kwa maana hata Rich Mavoco ameimba kwenye Wimbo wa Roho Yangu kuwa ‘ku….. ni siri ya ndani’ hivyo nao walifanye jambo hilo liwe siri.

Paulo na Angela waliwekwa kitako na wasamaria wema pamoja na mwenye
mke na kujadiliana jinsi ya kufanya ambapo awali Paulo alisema atampa
Ngosha faini ya Sh. milioni moja ili yaishe.
Wakati Ngosha akijiandaa kupokea kitita chake, alishangaa Paulo
alipomuambia fedha hiyo waandikishiane kimaandishi kwa kuwa hakuwa nayo
mkononi.
Ngosha aliona longolongo na kuomba msaada wa wasamaria wema wamsaidie kuwafikisha watuhumiwa wake polisi.

WAGONI WAPELEKWA POLISI MSOBEMSOBE
Mishale ya saa 7:42 usiku, wagoni hao walitembezwa mtaani wakipelekwa kituo cha polisi ambapo ilipofikia saa 8:34 usiku, walikuwa wamefikishwa Kituo Kidogo cha Polisi cha Buguruni Kwamnyamani, Dar.
Wakiwa kituoni hapo, baba mwenye nyumba wao alitoa lake la moyoni na kuwakabidhi wote waliofumaniana kituoni hapo na kujivua lawama.

Hata hivyo, hadi OFM inaondoka kituoni hapo, bado wahusika walikuwa wakihojiwa ili sheria ichukue mkondo wake.