WAKATI
hofu kubwa ikiwa imetanda miongoni mwa wananchi wa Wilaya za Butiama na
Tarime mkoani Mara kutokana na mauaji ya watu zaidi ya 16, imebainika
kwamba sababu za vifo hivyo zimejikita katika wivu wa kimapenzi, vitendo
vya ulipizaji visasa na imani za kishirikina.
Marehemu Juma Marwa Nyaitara.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka vyanzo mbalimbali mkoani humo, mauaji hayo,
hasa ya akina mama, yamekuwa yakifanyika mchana wakati wakiwa katika
shughuli za kilimo, kitu ambacho kimewafanya kuogopa mno na kubadili
hata ratiba ya kulala, kwani hivi sasa wanalala mapema zaidi.
Zacharia Chacha Mwita enzi za uhai wake.
“Kule
kijijini kwetu hali ni mbaya sana kiasi kwamba akina mama ambao ndiyo
waathirika wengi wa mauaji haya, wamekuwa na hofu kubwa kiasi cha
kuwafanya wasiende shambani pia wanalala mapema.
“Kwa
kipindi cha mwezi mmoja jumla ya watu nane wameuawa, lakini mpaka sasa
hakuna aliyekamatwa akihusishwa na matukio hayo, nafikiri jaribu
kuwasiliana na mwenyekiti wa kijiji chetu atakupa ukweli zaidi,”alisema
Mwita Marwa aliyedai ni mkazi wa Kijiji cha Mtiriri ambaye kwa sasa yupo
Dar.
Muuaji anadaiwa kuvaa vazi kama hili la Kininja.
Mwenyekiti
wa kijiji hicho, Pascal Maerere alikiri kuwepo kwa mauaji hayo na
kuwataja waliouawa kuwa ni pamoja na Nyabuturi Makanga ambaye mwili wake
ulikutwa porini Januari 10, mwaka huu ukiwa umechinjwa huku sehemu
ukiwa umeliwa na wanyama.
Wengine
waliouawa ni Upendo Manyama aliyevamiwa nyumbani kwake na kukatwa
mapanga hadi kufa Desemba 12, mwaka jana. Januari 6, mwaka huu, mwanaume
ambaye hakufahamika jina alikutwa shambani akiwa ameuawa.
Mkaguru
Magee, mwili wake ulikutwa wiki iliyopita ukiwa umefukiwa wakati Juni
8, mwaka jana, mtu moja aliyedaiwa kutoka Musoma mjini aliuawa na mwili
wake kukutwa na majeruhi. Polisi waliuchukua mwili huo ambao jina lake
halikujulikana.
Samwel Richard Mohenga (37) wa kijiji cha Rebu, Mara enzi za uhai wake.
Ziada
John, mkazi wa kijiji jirani cha Nyasurura, mwili wake ulikutwa katika
pori ukiwa umenyongwa kwa kutumia nguo yake wakati Nkwaya Busia, mkazi
wa kijiji hicho alienda kulima shambani kwake lakini baadaye mwili wake
ulikutwa ukiwa na alama ya kuchomwa kisu.
Mwingine
aliyejulikana kwa jina la mama Khadija, mkazi wa Musoma mjini naye
alikutwa amekufa kijijini hapo kwa kukatwa panga na mwili wake kuokotwa
porini Mei 28, mwaka juzi.
Mwenyekiti huyo alisema matukio hayo huenda yanatokana na mambo ya kishirikina, visa vya mapenzi, ujambazi au kisasi.
Mwenyekiti huyo alisema matukio hayo huenda yanatokana na mambo ya kishirikina, visa vya mapenzi, ujambazi au kisasi.
Marehemu Busia.
“Kwa kweli inauma sana, watu wanachinjwa kama kuku, wanapigwa risasi hadharani,” alisema kiongozi huyo.
Katika Wilaya ya Tarime, wananchi nane nao wameuawa na mtu mmoja anayejifunika uso kama ninja anayetumia bunduki aina ya SMG ambaye hadi sasa hajaweza kupatikana.
Katika Wilaya ya Tarime, wananchi nane nao wameuawa na mtu mmoja anayejifunika uso kama ninja anayetumia bunduki aina ya SMG ambaye hadi sasa hajaweza kupatikana.
Waliotajwa
kuuawa kwa risasi na mtu huyo anayehisiwa kutaka kulipiza kisasi na
ambaye anaripotiwa kuvaa Kininja ili kuficha sura ni Juma Mwita Mtodi
(68), Chacha Robert Kisiri (36), Chacha Marwa (58), Erick Lucas Mohabe
(24), Juma Mwita Nyaitara, David Yomani, Samwel Richard na Sami Magori
mwenye umri wa miaka 35.
Marehemu Upendo enzi za uhai wake.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mara, Frednand Mtui alikiri kupitia simu yake ya
mkononi kutokea kwa mauaji hayo na ili kupata dawa, ameshakutana na
viongozi wa dini, wananchi ili kuimarisha ulinzi kwa kila mtaa.
“Unajua
haya mauaji mara nyingi hutokea mchana, hasa kwa akina mama na
inawezekana mambo ya kishirikina yakawa yametawala, nimewaagiza kutoenda
shambani mtu mmoja mmoja na vijana wangu wanaendelea na uchunguzi wa
kina,” alisema Kamanda Mtui.