MRENO
Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia wa mwaka wa
FIFA kwa mara ya pili katika historia yake, akimuangusha mshindani wake
mkuu, Lionel Messi.
Nyota
huyo babu kubwa wa Real Madrid alikuwa anakabiliwa na ushindani wa
mbali kidogo kwa nyota wa Barcelona, Messi na wa Bayern Munich, Franck
Ribery katika kinyang'anyiro cha Ballon d’Or.
Akiwa
mwenye hisia kali, Ronaldo aliyekwenda jukwaani kuchukua tuzo yake
akiwa ameambatana na mtoto wake wa kiume, Cristiano alishindwa kujizuia
na kumwaga machozi wakati anapokea taji hilo.
Hisia: Ronaldo alishindwa kujizuia na akamwaga machozi jukwaani wakati anapokea tuzo ya Ballon d'Or
Mshindi: Pele akiwa amemshika mtoto wa Ronaldo, Cristiano wakati Mreno huyo anapokea tuzo yake
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 28 amepewa tuzo hiyo baada ya kufunga mabao
66 katika mechi 56 za klabu na nchi yake, Ureno mwaka 2013 hatimaye
kuirejesha tuzo yake aliyoitwaa awali mwaka 2008.
Pamoja
na kwamba Ronaldo hakutwaa taji kubwa mwaka 2013, alifunga mabao yote
manne Ureno ikiitoa Sweden katika kinyang'anyiro cha tiketi ya kombe la
Dunia baadaye mwaka huu.
"Hakuna maneno ya kusema wakati huu," Ronaldo alisema, huku akifuta machozi. "Nataka kuwashukuru wenzangu wote na washirika pale Real Madrid, katika timu ya Ureno na familia yangu, ambako wako nami,".
"Wale
ambao wananifahamu mimi, wanafahamu kwamba watu wengi wananisaidia:
kocha wangu, rais wetu, na sitaki kusahau kumtaja Eusebio. Mpenzi wangu
na mwanangu pia. Nasonga zaidi,".
Ronaldo na mpenzi wake Irina Shark katika sherehe za tuzo
Washindani: Ronaldo, Lionel Messi na Franck Ribery kabla ya sherehe
Gwiji Pele alipea tuzo katia usiku huo mjini Zurich
Mfalme wa soka: Gwiji wa Brazil, Pele alishindwa kujizuia kutoa machozi alipokuwa jukwaani
Retied
Jupp Heynckes ameshinda tuzo kocha bora wa mwaka wa dunia baada ya
kuiwezesha Bayern Muich kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya
Mkali: Zlatan Ibrahimovic ameshinda tuzo ya Bao Bora la mwaka, maarufu kama Puskas
Bao lake tik tak Sweden ikiifunga 4-2 England Novemba mwaka 2012 ndilo bao bora la mwaka
Kipa wa Ujerumani, Nadine Angerer ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa kike wa mwaka wa Dunia
Wawili: Ronaldo na Angerer baada ya kutajwa wanasoka bora wa dunia
Taji: Angerer alikuwemo kwenye kikosi cha Ujerumani kilichoshinda Kombe la ubingwa wa Ulaya kwa wanawake