Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete ametangaza kuwa kesho, Jumatatu, Januari 13, 2014, itakuwa ni
Siku ya Mapumziko (Public Holiday) kwa Watanzania wote kusheherekea
miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais Kikwete ameutangaza uamuzi huo mjini Zanzibar ambako leo
ameungana na Watanzania na Wazanzibari wote kusheherekea miaka 50 ya
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, mwaka 1964.
Mapinduzi hayo yaliyoongozwa na mwasisi wa Zanzibar na Taifa la
Tanzania, Hayati Abeid Amaan Karume yalifanikiwa kuung’oa madarakani
utawala dhalimu wa Sultan na kuwawezesha kwa mara ya kwanza katika
historia Waafrika walio wengine kujitawala ndani ya nchi yao wenyewe.
Yalikuwa ni Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofungua njia ya kuzaliwa kwa
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar – miezi mitatu baada ya Mapinduzi
hayo – Aprili 26, 1964.
Naye Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa
Ali Mohamed Shein ametangaza kuwa kesho itakuwa Siku ya Mapumziko
Tanzania Visiwani kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais Shein alitangaza mapumziko hayo wakati alipohutubia wananchi
kwenye Uwanja wa Michezo wa Amaan mjini Zanzibar katika kusherehekea
miaka 50 ya Mapinduzi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametangaza kuwa kesho, Jumatatu, Januari 13, 2014, itakuwa ni Siku ya Mapumziko (Public Holiday) kwa Watanzania wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Imetolewa na;
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS
Ikulu,
Dar es Salaam.
Januari 12, 2014
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS
Ikulu,
Dar es Salaam.
Januari 12, 2014