RAIS mstaafu, Ali Hassan Mwinyi leo atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za Maulidi Kimkoa, Dar es Salaam zinazofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Sikukuu
ya Maulid inaadhimishwa na waumini wa dini ya Kiislamu duniani kote,
ikiwa na maana ya kumbukumbu kuzaliwa kwa Mtume Muhamad(S.A.W).
Kitaifa,
sherehe hizo zinafanyika Kigoma na mgeni rasmi ni Rais Jakaya Kikwete.
Akizungumzia sherehe hizo, Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa
Salumu alisema zinaanza saa 2 leo usiku.
Alisema
zinatanguliwa na maandamano ya dini, yatakayopita mitaa mbalimbali ya
katikati ya Jiji la Dar es Salaam kuelekea katika viwanja hivyo. Ujumbe
wa Maulid ya mwaka huu ni ' Uislam kwa amani ya wote', ukilenga
kujulisha kuwa misingi ya dini hiyo ni amani.
Kwa
upande wake, Peti Siyame wa Sumbawanga anaripoti kuwa wakazi wa mkoani
Rukwa, wanatarajia kujiunga na Waislamu duniani kote kusherehekea Maulid
ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad katika mkesha ya maadhimisho hayo kwenye
Msikiti wa Masjid Nuru.
Kwa
mujibu wa Shehe wa Mkoa wa Rukwa ,Rashid Akilimali, mgeni rasmi ni Mkuu
wa Wilaya ya Nkasi, Iddy Kimanta. Shehe Akilimali alisema wageni kutoka
ndani na nje ya mkoa, wanatarajiwa kuhudhuria akiwemo, Naibu Katibu
Mkuu Taasisi ya Tablidh, Shehe Amir Lulu akitoka jijini Dar es Salaam.
“Kuanzia
kesho (leo) tunatarajia wageni kutoka wilaya zote mkoani hapa ikiwemo
kutoka maeneo ya Kirando (Nkasi ) , Kasanga (Kalambo) mwambao mwa Ziwa
Tanganyika kuanza kuwasili mjini hapa kwa ajili ya maadhimisho haya,”
alisema.
>>Habari leo
>>Habari leo