Taarifa zilizopatikana kutoka eneo la tukio na baadaye kufuatiliwa kwa karibu na waandishi wetu, zinasema mtoto huyo ambaye hafahamiki alikotokea, alionekana akishinda na kulala katika makaburi hayo kwa zaidi ya mwezi mzima uliopita, kabla ya kutoweka kuelekea sehemu isiyojulikana.
Lakini
baada ya siku kadhaa za kutoweka kwake, majirani wanasema walimuona
tena mtoto huyo akiendelea na maisha eneo hilo ndipo walitoa taarifa
Kituo Kidogo cha Polisi Yombo kuwataarifu juu ya tukio hilo lisilo la
kawaida.
Polisi walifika makaburini hapo na kumchukuwa kijana huyo lakini walipomuhoji hakuweza kuongea chochote, hali iliyowafanya askari hao kutojua cha kufanya.
Kutokana
na hali hiyo, polisi wa Kigilagila walifanya mawasiliano na Kituo cha
Buguruni kwa hatua zaidi, ikiwemo kubaini anakotoka na sababu za kuishi
katika mazingira hayo.
Paparazi
wetu alimfikia na kumkuta mtoto huyo akiwa katika Kituo cha Buguruni
anakohifadhiwa wakati ndugu au wazazi wakisubiriwa, kabla ya taratibu
za kumkabidhi kwa Ustawi wa Jamii kuanza kuchukuliwa.
Aidha,
vyanzo vyetu ndani ya kituo hicho vilisema kuna watu walijitokeza
wakiwa wanatafuta mtoto wa namna hiyo, lakini baada ya kumuona, walisema
hakuwa yeye.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, SACP Marietha Minangi alithibitisha
kuwepo kwa mtoto huyo na kwamba taratibu zinafanywa ili kulimaliza
tatizo lake.
“Natoa
wito kwa wananchi waliopotelewa na kijana mwenye umri huo, kufika
katika Kituo cha Polisi Buguruni ili kuweza kumtambua mtoto huyo,”
alisema Kamanda Minangi.