VIDEO: MDOGO WAKE DIAMOND ATOA VIDEO YA KUONYESHA MAISHA YA DIAMOND KABLA HAJATOKA..


Tazama video ya magoli ya Simba vs Kagera sugar na fujo zilizotokea uwanjani..



1October 31 2013 kulikua na mechi ya Simba vs Kagera Sugar kwenye uwanja wa taifa ambapo timu hizo zilitoka 1-1 huku goli lililoleta malalamiko likiwa ni la Kagera Sugar ambalo lilifungwa kwa njia ya penat.
Kocha wa Kagera Sugar amesifia maamuzi ya refa na kusema ‘nafurahi timu imesawazisha kwenye dakika za mwisho na refa amefanya kazi yake kwa sababu ni siku nyingi sana marefa hawagawi penat kama hizo, timu nzuri inacheza mpaka goli’
Kocha Kibaden wa Simba kasema ‘nashukuru tumemaliza mpira salama na vijana wametoka salama, sijafurahishwa na jinsi mpira ulivyochezeshwa, sitaki kusema hayo kwa sababu watu wana macho na wanaweza kukosoa lakini uamuzi haukuwa sawasawa, kama tutaendelea na mpira wa aina hii nafikiri tutaondoka kwenye mwelekeo… naomba TFF mpya iliyokuja ijaribu kutazama watu wapumbavu wa aina hii wanaokuja pale kuwaudhi watu, sijafurahishwa na mpira ulivyochezeshwa mwanzo hadi mwisho na nilijua kitatokea nini’

NUSU UTUPU YA LINAH YAWADATISHA WANAUME..!


Linah akiwa jukwaani wakati wa shoo ya Fiesta 2013 jijini Dar.

Mavazi ya nusu utupu ambayo msanii Esterlina Sanga ‘Linah’ hupenda kuyavaa hasa kwenye matamasha yamekuwa yakiwadatisha wanaume na wengine kuomba kupiga naye picha kwa lengo la ‘kujipoza’ kama ilivyotokea kwenye Fiesta, Dar hivi karibuni.
 

 
Linah akipozi na baadhi ya wanaume walioomba kupiga naye picha.
 
Ijumaa limekuwa likimfuatilia Linah na kubaini kuwa kila mara hupenda kuvaa nguo zinazoacha wazi mapaja na kitovu chake na watu ambao amekuwa akipiga nao picha ni wanaume ambao wengi huonekana wakiwa wamemshika kimahaba.

Hata hivyo, licha ya mwenyewe mara kadhaa kueleza kuwa, hayo ni mvazi ya kikazi zaidi, baadhi ya mashabiki wamemponda na kumtaka kubadilika hasa ikifahamika kuwa ni mtoto aliyetokea kwenye familia iliyoshika dini na kwamba kuvaa hivyo ni kujidhalilisha. 
GPL

PAMOJA NA MISHAHARA YAO WABUNGE ....! JE NI HALALI KWAO KULALAMIKA MASLAHI MADOGO..??


Imethibitika rasmi kuwa wakati wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania wakilalamikia maslahi madogo, mbunge mmoja hulipwa mshahara wa Sh. milioni 11 kwa mwezi.

Kiasi hiki hakijumuishi posho ya Sh. 330,000 anayolipwa mbunge kwa kuhudhuria kikao kimoja kwa siku. Posho ni Sh. 80,000 za kujikimu akiwa nje ya jimbo lake, posho ya vikao Sh. 200,000 kwa siku na mafuta ya gari Sh. 50,000, jumla kuwa Sh. 330,000 kwa siku.

Aidha, mbunge mmoja hulipwa ‘gratuity’ (kiinua mgongo au bahashishi) ya Sh. milioni 72 baada ya kumaliza kipindi chake cha miaka mitano cha ubunge.

Aidha, wabunge hupewa fedha za Mfuko wa Jimbo Sh. milioni 30 kila mwaka kwa ajili ya kusaidia shughuli za maendeleo katika majimbo yao.

TAZAMA VIWANGO VIPYA VYA ALAMA ZA UFAULU WA ELIMU YA SEKONDARI..SOMA HAPA...!



UPANGAJI WA VIWANGO VYA ALAMA, MATUMIZI YA ALAMA ENDELEVU YA MWANAFUNZI NA UFAULU

UTANGULIZI

Wizara imekusanya maoni ya Wadau wa Elimu kuhusu Upangaji wa Viwango vya Alama (Grade Ranges) katika Mitihani ya Kuhitimu Kidato cha Nne na cha Sita pamoja na Matumizi ya Alama za Tathmini Endelevu ya Mwanafunzi (Continuous Assessment ama CA) kwa ajili ya kuamua kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi. 

Maoni ya wadau yamekusanywa kwa sababu kwa muda mrefu sasa upangaji wa viwango vya alama vinavyotumika na utaratibu wake katika mitihani ya kuhitimu Kidato cha Nne na Kidato cha Sita umekuwa haufanani pamoja na kwamba mitihani hiyo yote ni ya elimu ya sekondari. 

Pia mfumo masuala mbalimbali ya mitihani katika elimu ya sekondari umekuwa na miundo tofauti ikiwemo ule unaotumika shuleni na ule wa Baraza la Mitihani la Taifa. Kwa sasa kuna miundo mikuu miwili katika mfumo huo.

Muundo wa Kwanza ni upangaji wa viwango katika ngazi ya Shule ambapo Alama Mgando (Fixed Grade Ranges) zifuatazo  hutumika kupanga madaraja: A = 81 – 100; B = 61 – 80; C = 41 – 60; D = 21 – 40 na F = 0 – 20. Muundo huu umetumika kwa muda mrefu na umezoeleka kwa walimu na wanafunzi wa elimu ya sekondari kwa ujumla.

Muundo wa Pili ni wa viwango vinavyotumiwa na Baraza la Mitihani la Taifa ambapo ambapo kabla ya mwaka 2012 muundo wa viwango nyumbufu (flexible grade ranges) ulitumika. 

Katika muundo huu uwigo wa alama ulibadilika badilika kulingana na hali ya matokeo ilivyokuwa kwa mwaka husika. Lakini kuanzia mwaka 2012, Serikali iliamua kutumia mfumo wa Upangaji wa Alama Mgando (Fixed Grade Range) kwa Kidato cha Nne na Kidato cha Sita. 

Katika mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012 Baraza lilitumia mfumo huu wa alama mgando ambapo: A = 80 – 100, B = 65 – 79, C = 50 – 64, D = 35 – 49, F = 0 – 34. 

Kwa upande wa Kidato cha Sita Baraza lilitumia mfumo wa A = 80 – 100; B = 75 - 79; C = 65 – 74; D = 55 – 64; E = 45 – 54; S = 40 – 44 na F = 0 – 39. 

Mifumo hii ya Baraza haikuwa inafahamika kwa wadau na hivyo kuwa sehemu ya malalamiko katika sekta ya elimu na mafunzo.

Vilevile, Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995 imeelekeza kwamba katika kuamua kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi wa elimu ya sekondari, Alama za CA zitachangia asilimia hamsini (50%) na Mtihani wa mwisho utachangia asilimia hamsini (50%). 

Kwa upande wa Zanzibar, CA zimekuwa zikiandaliwa kwa mfumo wa asilimia arobaini (40%) na mtihani wa mwisho asilimia sitini (60%). Pamoja na kwamba Baraza halijawahi kuutumia mifumo hii tangu ilipowekwa, kumekuwa na mitazamo, maoni na mapendekezo tofauti katika muundo na matumizi ya alama za CA

Kuna mawazo pia kwamba mfumo wa CA kuchangia matokeo ya mwisho ya mwanafunzi pia utumike kwa watahiniwa wa kujitegemea (private candidates). 

Kwa sasa matokeo ya mitihani ya watahiniwa hawa yamekuwa yakitumia alama za mtihani wa mwisho tu na hivyo kutafsiriwa kama utaratibu ambao unamwonea mwanafunzi ambaye anahamu ya kujiendeleza kielimu lakini anakwama kwa sababu mfumo unaotumika siyo rafiki kwa mtahiniwa.

Kwa mantiki hii, Wizara imedhamiria kufanya harmonization ya masuala ya alama katika mitihani ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita ili kupata muundo mmoja na ulio wazi kwa wadau wote wa elimu ya sekondari. 

Lakini pia serikali imedhamiria kuhakikisha tathmini za wanafunzi katika ngazi mbalimbali zinakwenda sambamba na matarajio ya mitaala inayotumika na ambayo inahuishwa mara kwa mara ili iendane na wakati na mahitaji ya elimu katika ngazi mbalimbali.

VIWANGO NA UTARATIBU KUANZIA MWAKA 2013 KWA KIDATO CHA NNE NA KIDATO CHA SITA  KWA MWAKA 2014

Baada ya kufanya tathmini ya maoni mbalimbali ya wadau, misingi ifuatayo ilizingatiwa katika maamuzi kuhusu makundi ya alama na muachano wake:

a)     Alama zitakazotumika zitakuwa A, B, C, D, E na F. Muachano wa alama kati ya kundi moja hadi jingine utafanana, isipokuwa tu pale ambapo itaonekana kuna sababu na hakuna athari za kuwa na muachano tofauti na ule ambao umetumika katika makundi mengine.

b)    Makundi ya alama hayatakuwa na clusters isipokuwa pale ambapo itaonekana kufanya hivyo kunaleta tija katika kupata picha ya wahitimu kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Kwa mantiki hii

(i)      makundi ya alama A, C, D, E na F yabaki na cluster moja moja bali kundi la alama B litakuwa na clusters mbili. Kundi la kwanza litakuwa la wale ambao wamepata alama kati ya 50 mpaka 59 na litaitwa B na lingine litakuwa la wale ambao wamevuka uwigo wa 50 hadi 59 na kuelekea uwigo wa 60 hadi 74 na hili litaitwa B+ (angalia jedwali hapo chini).

(ii)     Pamoja na kuwa na muachano wa alama 26 kama jedwali linavyoonesha hapo chini, alama A kwa miaka mingi imekuwa ikianzia alama 75 hadi 100 na kwamba pamoja na uwigo huo bado wanaofaulu kwa kiwango hicho ni wachache sana. 

Kwa mantiki hii, hakuna haja ya kubadilisha uwigo ila juhudi ziendelee katika ufundishaji na ujifunzaji ili kiwango cha ufaulu kiongezeke na kupata wanafunzi wengi zaidi wanaofaulu katika kundi hili.

(iii)    Pia, pamoja na kuwa na muachano wa alama 20 kama jedwali linavyoonesha hapo chini kwa miaka mingi, huko shuleni mwanafunzi aliyepata alama 21 na hadi 30 alihesabiwa kuwa na ufaulu wa chini kabisa au hafifu kwa kiwango cha alama D na ingawa ilikubalika ufaulu wa aina hiyo kwa mazingira ya nchi yetu unaridhisha.

 Alama Filikuwa ni kwa wale waliopata chini ya hapo. Hivyo, alama F itaendelea kuwepo na itaanzia alama 0 hadi 19 na E itaanzia alama 20 hadi 29 na D – 30 -39. 

Lengo la muundo huu ni kuwa alama mbalimbali, isipokuwa kwa makundi machache, zianzie kwenye 0 yaani 0, 10, 20, 30, 40 na kuendelea badala ya kuanzia kwenye moja yaani 1, 11, 21, 31, 41 na kuendelea. 

Hii ni kwa ajili ya kuleta mtizamo unaofanana katika ngazi mbalimbali za elimu ambapo kwa sasa ngazi ambazo siyo za elimu msingi na sekondari zinatumia muundo wa kuanzia kwenye 0 badala ya 1.

c)     Uwigo wa jumla wa alama kwa Kidato cha Nne na Kidato cha Sita utaendelea kuwa wa alama 0 hadi 100 na kila kundi katika uwigo huu limepewa tafsiri kwa ajili ya kuamua mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya mwanafunzi kulingana na malengo ya mtihani husika. Kimsingi, tafsiri zifuatazo zitakatumika

(i)      Alama A itakuwa na maana ya ufaulu uliojipambanua (distincion or outstanding performance),

(ii)     Alama B+ itakuwa na maana ya ufaulu bora sana (excellent performance),

(iii)    Alama B itakuwa na maana ya ufaulu mzuri sana ( very good perfomance),

(iv)    Alama C itakuwa na maana ya ufaulu mzuri (good performance);

(v)     Alama D itakuwa na maana ya ufaulu wa wastani (low performance),

(vi)     Alama E itakuwa na maana ya ufaulu hafifu (very low performance), na

(vii)   Alama F itakuwa na maana ya ufaulu usioridhisha (unsatisfactory performance).

Wataalamu katika maeneo mbalimbali ya elimu na ulimwengu wa kazi, kwa kushirikiana na Wizara, watatoa maana ya tafsiri hizi kiutendaji katika maeneo yao kulingana pia na mahitaji yao.

d)    Alama C iwe ndiyo alama ya ufaulu mzuri ambao hauhitaji urekebu wa lazima, wakati alama D na E ni alama za ufaulu unaohitaji urekebu kadri mwanafunzi atakavyokuwa anaendelea na masomo ili kuthibitisha kama mlengwa anaweza na kulingana na mahitaji ya eneo husika (targeted remediation). 

Alama F iwe alama ya eneo linalohitaji urekebu wa hali ya juu (intesive remediation) ili mwanafunzi huyo aweze kumudu masomo kadri anavyoendelea kukua kielimu ama atakapoingia katika ulimwengu wa kazi.

e)     Makundi ya alama yatajumuisha CA kwa kiwango cha asilimia isiyozidi 40 na mtihani wa mwisho kwa asilimia isiyozidi 60 kwa makundi yote ya watahiniwa ikiwemo wale wa kujitegemea (private candidates). 

Hii ni kwa kuzingatia kwamba CA siyo vizuri izidi uwigo wa alama ya ufaulu mzuri unapoanzia ambayo ni C au 40.

f)      CA kwa upande wa Kidato cha Nne zitokane na mtihani wa Kidato cha Pili (alama 15), matokeo ya Kidato  cha Tatu (alama 5 kwa kila muhula, na hivyo jumla ya alama 10), mtihani wa Mock (alama 10) na kazi mradi  au Projects (alama 5). 

Kwa upande wa Kidato cha Sita, CA iendelee kutokana na muundo unaotumika sasa.

g)     CA zitumike pia kwa watahiniwa wa kujitegemea. Kwa upande wa watahiniwa wa kujitegmea ambao wanarudia Mitihani, CA zao  zitumike zile zilizotumika kutoa matokeo yake ya mitihani ya awali. 

 Kwa watahiniwa wa kujitegemea waliopitia mfumo wa Qualifying Test (QT), matokeo ya QT yatumike kama CA na mtihani wa mwisho uchangie alama 60.

h)    Kwa vile alama endelevu kwa mwaka 2013 kwa wanafunzi wa Kidato cha Nne tayari zimeshawasilishwa Baraza la Mitihani  Tanzania, alama hizo zichangie asilimia 40 katika mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2013.

i)       Muundo wa wastani wa alama katika ufaulu (Grade Points Average ama GPA) utaandaliwa na kuanza kutumika pale utakapokuwa tayari na wadau wataelimishwa kuhusu muundo huo ili wapate kuufahamu na manufaa yake katika elimu ya sekondari.

j)       Muundo huu mpya wa alama utatumika kwa mzunguko wa miaka minne kabla haujahuishwa tena ili kuupa muda wa kutosha kuona aina ya changamoto zinazojitokeza na jinsi ya kuzishughulikia. 

Aina hii ya muda itaruhusu vidato vinne vya elimu ya sekondari ya kawaida na nane ya elimu ya sekondari ya juu kupimwa. 

Hata hivyo, uhusihaji wa masuala ya mitihani unaweza ukafanyika iwapo matokeo ya uhuishaji wa mitaala kwa ujumla utahitaji pia eneo la mitihani liguswe na kuhuishwa pia.

Kwa mantiki hii, viwango vya alama na ufaulu ni kama inavyooneshwa kwenye jedwali la 1 hapa chini:

Jedwali Na 1

MUUNDO WA ALAMA NA UFAULU


ALAMA UWIGO WA ALAMA IDADI YA ALAMA TAFSIRI
A 75 - 100 26 Ufauli Uliojipambanua
B+ 60 - 74 15 Ufaulu bora sana
B 50- 59 10 Ufaulu mzuri sana
C 40 - 49 10 Ufaulu mzuri
D 30 - 39 10 Ufaulu Hafifu
E 20 - 29 10 Ufaulu hafifu sana
F 0 - 19 20 Ufaulu usioridhisha

Kwa aina hii ya muundo wa alama, na kwa kuwa muundo wa GPA utaanza kuandaliwa na wadau kuelimishwa kabla haujaanza kutumika, katika kipindi hiki mpaka wakati huo, muundo wa madaraja utakuwa kama inavyooneshwa kwenye jedwali la 2 hapa chini.

Jedwali Na 2

MUUNDO WA MADARAJA


MUUNDO WA ZAMANI MUUNDO MPYA MAELEZO
POINTI DARAJA POINTI DARAJA
7-17 1 7-17 I Kundi la ufaulu uliojipambanua na bora sana
18-21 II 18-24 II Kundi la ufaulu mzuri sana
22-25 III 25-31 III Kundi la ufaulu mzuri na wa wastani
26-33 IV 32-47 IV Kundi ufaulu hafifu
34-35 0 48-49 V Kundi la ufaulu usioridhisha

Wataalamu wa mifumo ya mitihani watalifanyia kazi zaidi jedwali hili la madaraja ili liweze kutumika kwa ufanisi katika kipindi hiki cha mpito.

Kwa mantiki hii, Daraja Sifuri linafutwa na kuwekwa daraja litakalojulikana kama Daraja la Tano na ambalo litakuwa ndilo la mwisho kabisa katika ufaulu.

HITIMISHO

Mabadiliko haya yamefanyika ili kuendelea kuimarisha mfumo wetu wa elimu na kuweka wazi taratibu mbalimbali kwa ajili ya mitihani na masuala mengine. 
Yako mambo mengi mengine ambayo hayana budi kuendelea kuimarishwa ikiwemo mfumo wa mitaala, walimu, mazingira ya kujifunzia na kufundishia pamoja na vitabu na vifaa vingine muhimu katika elimu.

 Masuala haya yanaendelea kuangaliwa kupitia mikakati mbalimbali ikiwemo mpango wa Matokeo Makubwa Sasa ama Big Results Now (BRN).
 Ushirikiano wa wadau wote ili kuleta tija kwenye elimu ni muhimu sana na hivyo wizara itaendelea kuwashirikisha wadau wote kwa kadri itakavyohitajika na wadau pia wanaombwa wasiache kuishirikisha wizara pale watakapokuwa na jambo lolote ambalo linahitaji ushirikiano ili kwa pamoja tuweze kupata mafanikio katika sekta ya elimu.

Imetolewa na,

KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

BINTI AAMUA KUJINYONGA MPAKA KUFA MARA BAADA YA WAZAZI WAKE KUMKATAZA ASITUMIE FACEBOOK NA AZINGATIE MASOMMO ZAIDI...!!

 Binti wa miaka 17 nchini India katika jiji la Parbhani amejiua baada ya wazazi wake kumkataza asitumia ukurasa wa Facebook ili apate muda wa kuzingatia masomo aliyokuwa akishindwa vibaya darasani tofauti na ilivyokuwa kabla yajaanza kutumia Facebook ambapo alikuwa akifaulu.


Aishwarya Dahiwal alikutwa ananing'inia chumbani kwake baada ya kuzuka mabishano baina yake na wazazi wake ambao 
walikuwa wanakerwa na muda mwingi anaoutumia kwenye mtandao wa Facebook na mazungumzo marefu kwenye simu yake ya mkononi.

Gazeti tando la habari za teknolojia, Gawker limeripoti kuwa marehemu aliacha ujumbe usemao kuwa asingweza kuishi bila mitandao ya kijamii na moja ya yaliyoandikwa humo ni pamoja na kuuliza, "Je, Facebook ni mbaya hivyo?"
"Siwezi kuishi katika nyumba yenye vizuizi vya aina hii na siwezi kuishi bila Faceboook" na hivyo kuwalaumu wazazi wake kwa hatua ya kujiua aliyoichukua.

Kama ilivyo kwa wazazi wowote ambao kwa kawaida wameyaona maisha na kufahamu mbinu za kukabiliana nayo, walikuwa na nia njema ya kutaka kumsaidia mtoto wao aweze kufanikiwa lakini mabadiliko ya kila kizazi yanayokuja na changamoto zake ambazo hazina vigezo wala vielelezo vya namna ya kumsaidia mtoto akabiliane navyo vyema hali akiyamudu maisha kwa uwiano, walijikuta katika huzuni ya kulazimika kukubaliana na jambo ambalo hawakutarajia lingetokea.

Bila shaka ujio wa internet umebadili maisha ya vijana na familia kwa ujumla. Pamoja na kuwa na faida nyingi kwa wale wanaojua namna ya kuitumia vyema, bado madhara na hasara zake ni kubwa ambazo zinaonekana dhahiri kwenye mahusiano ya aina zote iwe kikazi, kifamilia, kijamii au hata kutoka kwa mtu msiyefahamiana kabisa ila kwa kuwa amekuona kwenye moja ya mitandao ya kijamii, anaweza kukutisha na hata kukudhuru.

Jirani yangu alinisimulia jinsi rafiki yake alivyoibiwa nyumbani kwake baada ya kuandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa baada ya uchovu wa kazi wiki nzima, amekwenda kubarizi ufukweni na atarudi majira ya jioni hivi, kwa kuwa anwani yake ilikuwa kwenye wasifu wake (profile details) basi taarifa hizo zikawa maelezo ya kutosha kwa wezi kufanya watakavyo.

JE UNAZIFAHAMU KAULI ZA HATARI KWENYE MAPENZI....!! SOMA HAPA KUZIFAHAMU, USIJE UKAACHWA KWA KAULI ZAKO..

WAKATI fulani kwenye uhusiano suala la migogoro ni la kawaida. Inaelezwa kwamba, wapenzi wanapoingia kwenye kuhitilafiana ndiyo uimara wa penzi unapotokea.



Yeah! Matatizo hukomaza akili. Mkikaa bila kugombana ni vigumu kujua namna mwenzako alivyo hasa kama ikitokea kutoelewana baadaye.
Rafiki zangu, kugombana hakuna maana ya kumalizika kwa uhusiano hasa kwa wale walio kwenye ndoa. Mambo yanatokea, yanatatuliwa na mwisho wake maisha yanaendelea kama kawaida.
Kwa bahati mbaya sana ni kwamba, wengine wanapokuwa kwenye migogoro na wenzi wao, badala ya kutafuta njia za utatuzi, wanazalisha tatizo lingine!
Jambo la kusikitisha ni kuwa, tatizo jipya linalozaliwa linaweza kusababisha matatizo makubwa zaidi katika uhusiano huo na mwisho wake kusababisha kuachana kabisa.
Ngoja tupanue mawazo yetu leo hapa, Zipo kauli ambazo ukizitoa kwa mpenzi/mke/mume wako wakati mkiwa kwenye ugomvi, zinaweza kuzalisha tatizo kubwa zaidi mbeleni.


KWA NINI KAULI?
Inawezekana ukajiuliza; ni kwa nini nimesema kauli? Rafiki zangu, kwa kawaida, watu wakiwa kwenye ugomvi, jambo kubwa linalotokea ni kutupiana maneno.
Katika hali hiyo basi, kwa wenzi au wanandoa ni vyema kuchunga ndimi zao maana zinaweza kusababisha matatizo makubwa siku zijazo. Baadhi ya Kauli hizo na kama zifuatazo hapa chini...

‘HUNA AKILI’
Wako baadhi ya watu wakigombana (hasa wanaume) wamekuwa na tabia ya kuwaambia wanawake wao: “Wewe huna akili kabisa...yaani hutumii akili kabisa katika kufanya mambo yako.
“Unakurupuka tu. Sasa ishu kama hii, hata mtoto mdogo anajua ni makosa, inakuwaje wewe unakosea?”
Hili ni jeraha la moyo. Mwanamke ukimwambia hana akili anajisikia vibaya, unampa kovu kubwa moyoni mwake. Anajiona wa hali ya chini na anahisi ameshuka thamani yake.
Kwake, kumwambia hana akili, ataanza kuwaza kuwa yupo mwanamke mwingine ambaye kwako ana akili kuliko yeye. Ni maumivu makali sana kwake.

‘NITAKUACHA’
Baadhi ya wanaume wana ulemavu huu. Ugomvi kidogo tu, atamwambia mwenzake: “Endelea na tabia zako za hovyo, ipo siku utajuta. Nimevumilia mengi sana lakini kuna siku nitachoka.
“Hutaamini macho yako. Siyo lazima niishi na wewe. Siwezi kuendelea kuteseka nikiwa na wewe. Nitakuacha nakuambia ukweli.”
Hii ni kauli mbaya ambayo inapandikiza chuki ndani ya moyo wa mwanamke. Kwanza kwa kumwambia hivi, hata kama alikuwa hakusaliti, unamfanya aanze kufikiria kutafuta mtu mwingine wa kumliwaza.
Kauli hii hasa kama ukiirudia zaidi ya mara mbili, humkaa akilini mwake na huanza kuwaza kuhusu kuwa na mwanaume mwingine nje ili apate mahali ambapo hata kama ukimuacha, atapata pumziko la uhakika.

‘NAKUVUMILIA TU’
Ni kweli mapenzi ni uvumilivu. Kuvumiliana ni siri ya uhai wa ndoa nyingi lakini hilo linapaswa kubaki moyoni.
Kugombana na mwenzako halafu umwambie kuwa unamvumilia tu, inamaana kwamba kuna siku uvumilivu wako utaondoka na utafanya maamuzi magumu – kuachana!
Si kauli njema kwa mwenzi wako. Mbaya zaidi humfanya aanze kufanya maandalizi ya mtu wa kuziba nafasi yako hata kama ni kwa usaliti.

‘KUNA SIKU UTAJUTA’

Kauli hii haina tofauti kubwa sana na iliyotangulia maana kinachofanyika hapa ni kumuandaa mwenzi wako kwa ajili ya matatizo siku zijazo.
Kumwambia: “Kuna siku utajuta, endelea na mambo yako tu, utaona.” Hii inamaanisha kwamba, uamuzi ulio ndani yako si mzuri kwake lakini ni suala la muda tu.
Ataamini (na ndivyo ilivyo mara nyingi) kuna muda ambao atajuta sana kwa sababu yako.
Hiyo ni sawa na kutengeneza bomu unaloliandaa kulilipua muda ujao.
Hizi ni baadhi ya kauli ambazo ni wapenzi wengi wanapenda kuzitumia wakati wa malumbano, lakini zina madhara makubwa sana katika maisha ya baadae ya mahusiano yenu kwahiyo chunga sana unapogombana na mpenzi wako kauli zakumwambia....


WAPENZI: JE MPENZI WAKO AMEKUSALITI..?? SOMA HAPA KUFAHAMU HATUA KUMI ZA KUCHUKUA BAADA YA KUSALITIWA...


Katika maisha ya kimapenzi hakuna kitu kinachouma kama kusalitiwa, tena kusalitiwa kunakouma zaidi ni pale unapobaini mpenzi wako kampa penzi mtu unayemjua halafu ukijilinganisha wewe na huyo aliyepewa unashindwa kuelewa kilichomshawishi mpenzi wako.
Lakini licha ya kwamba usaliti si kitu kizuri, watu wamekuwa wakisalitiana, tena sana tu. Inafika wakati unashindwa kuamini kama yupo mtu ambaye hajawahi kumsaliti mpenzi wake.
Niseme tu kwamba wapo wachache waliotulia ila asilimia kubwa ya walio kwenye uhusiano ni wasaliti hata tafiti zimethibitisha hilo. Kama hali yenyewe iko hivyo, cha kujiuliza ni kwamba unapobaini mpenzi wako kakusaliti ni kipi unachotakiwa kufanya? Je, ni kuamua kunywa sumu kama ambavyo wamekuwa wakifanya wengine? Sidhani kama huo ni uamuzi sahihi.
Mtaalam wa masuala ya mapenzi James Johnson kutoka Marekani amependekeza mambo 10 unayoweza kufanya baada ya kubaini kuwa mpenzi wako amekusaliti.

1. Kubaliana na kilichotokea
Kama kishakusaliti ni tukio ambao limeshatokea na haliwezi kufutika. Kubali kuwa umetendwa, huzunika lakini mwisho liache lipite ili uweze kujipanga upya.

2. Usijilaumu

Wapo ambao wakishasalitiwa hujuta kukubali kuingia kwenye uhusiano na watu waliowatenda. Utamsikia mtu akisema ‘najuta kumkubalia awe mpenzi wangu’. Kujilaumu kwa namna hiyo hukutakiwi kwani kutakufanya uzidi kunyong’onyea.

3. Jitoe

Jifanye kama vile aliyesalitiwa siyo wewe bali ni rafiki yako kisha jiulize ungemshaurije? Ushauri ambao ungempata basi uchukue kisha uufanyie kazi.

4. Pima ulivyoathirika

Je, kitendo cha mpenzi wako kukusaliti kimekukosesha imani juu yake? Kama ni hivyo, unadhani una sababu ya kuendelea kuwa naye au unahisi madhara aliyokupatia huwezi kumvumilia?

5. Mpasulie ukweli

Kwa vyovyote utakavyoamua ni lazima umweleze juu namna alivyokuumiza kwa usaliti wake. Hata kama utampa nafasi nyingine lazima ajue jinsi alivyokuumiza ili iwe changamoto kwake.

6. Chunguza kwa nini kakusaliti

Usiliache likapita hivi hivi, unatakiwa kujua sababu ya yeye kukusaliti. Je, kuna ambacho anakikosa kwako au ni tamaa zake tu? Jibu utakalolipata litakusaidia katika maisha yako ya kimapenzi.

7. Usikubali akulainishe

Huenda huyo mpenzi wako ni ‘msanii’ na anaweza kukulainisha kwa maneno ambayo yanaweza kukufanya ukalichukulia tukio hilo kiurahisi. Kuwa na msimamo na eleza hisia zako kwa uwazi.

8. Amua kusuka au kunyoa

Likishatokea hilo jaribu kuzungumza na moyo wako. Uamuzi wa kuendelea kuwa naye au kumuacha uuchukue bila shinikizo. Hata kama kakuumiza, kama unadhani unaweza kumpa nafasi nyingine mpe ili usije ukajuta baadaye kwa kumkosa lakini kama unaona moyo wako unamkataa, muache.

9. Msamehe

Kwa uamuzi wowote utakaochukua ni lazima uwe tayari kumsamehe ili kuliondoa dukuduku lako rohoni. Kutokumsamehe kunaweza kukufanya ukawa unaumia kila wakati na kukosa amani.

10. Iwe fundisho kwako

Chukulia tukio hilo kama fundisho kwako. Huenda wewe ndiye uliyechangia kusalitiwa, kama ni hivyo badilika ili yasije yakakukuta kama hayo utakapokuwa na mwingine. Pia kama kusalitiwa kumetokana na kutoridhika kwa mpenzi wako, kuwa makini wakati wa kuchagua mwingine wa kuwa naye.

AFIA MAHAKAMANI AKISUBIRI KUMWEKEA DHAMANA MTOTO WAKE....

 

MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Tiger Mwaigomole (70) Mkazi wa kata ya Masukulu wilayani Rungwe amefariki dunia ghafla akiwa katika chumba cha Mahakama ya Wilaya ya Rungwe akifuatilia mwenendo wa kesi inayomkabili mtoto wake wakati Mahakama ikiendelea.

Tukio hilo la aina yake lilitokea hivi karibuni majira ya saa 9 alasiri ndani ya Mahakama hiyo ambapo Marehemu alifika mahakamani hapo akiwa na mwanaye aliyejulikana kwa jina la Lusajo Tiger (40) wakiwa na lengo la kumwekea dhamana ndugu yao Gwakisa Tiger ambaye alifikishwa mahakamani hapo akituhumiwa kwa kosa la kupigana na kujeruhi katika ugomvi uliotokea kijijini kwao.

Kwa mujibu wa mtoto wa Marehemu aliyekuwa ameongozana nae Mahakamani hapo Lusajo Tiger alisema wakati kesi ikiendelea chini ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Rungwe, Kingwele, ndugu yao alipandishwa kizimbani kusomewa mashtaka yanayomkabili ndipo marehemu alipoanza kutetemeka kwa madai kuwa anajisikia baridi kali sana.

Alisema kutokana na marehemu kulalamikia baridi aliamua kumnunulia chai ya moto ili anywe na kupunguza baridi ambapo baada ya kufanya hivyo marehemu alikata roho muda mfupi baada ya kumaliza kunywa chai aliyokuwa amepelekewa huku akiwa amekaa ndani ya chumba cha mahakama hiyo.

Kutokana na tukio hilo Askari polisi waliokuwepo mahakamani hapo waliuchukua mwili wa marehemu na kuukimbiza katika Hospitali ya Wilaya ya Rungwe Makandana kwa ajili ya vipimo lakini hata hivyo mwili ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi ingawa ripoti ya kifo chake haikutolewa mapema.

Wakati huo huo Hukumu ya kesi ya mauaji dhidi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Rungwe, John Mwankenja inayowakabili Hakimu Mwakalinga na wenzie watatu huenda ikatolewa Novemba 11 mwaka huu baada ya Mahakama kuu kanda ya Mbeya chini ya Jaji Samwel Karua kumaliza kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka pamoja na utetezi kwa upande wa watuhumiwa.

Kwa mujibu wa Jaji Karua alisema baada ya kumaliza kusikiliza pande zote mbili atatumia muda wa siku mbili kwa ajili ya kuandika hukumu ambayo itaitoa Novemba 11, Mwaka huu, kesi ambayo inasimamiwa na Mwanasheria wa Serikali Archiles Mulisa huku watuhumiwa wakitetewa na Mawakili wawili wa kujitegemea ambao ni Simon Mwakolo na Victor Mkumbe.
Na Mbeya yetu

LAANA...!! PICHA ZA UCHI ZA MSANII NYOTA WA BONGO MOVIE AKICHEZEWA NYETI ZAKE NA WANAWAKE ZANASWA...

 

Mmh wimbo la mastaa wetu kuendelea kujishushi hadhi linaendelea kushika kasi kila kukicha huku hakuna sheria zozote zinazochukuliwa dhidi yao. 

Msanii nyota toka kiwanda cha bongo movie Edward Tem "Nick" picha zake za utupu zaidi 200 zimenaswa na mtandao huu hatari   zikimuonesha akiwa na wanawake zaidi ya watano amabao wanasadikika kuwa machangudoa wakimchezea nyeti zake. 

Hapa tumeziweka baadhi ya picha tu ili tupate kujifunza kupitia vitendo viovu wanavyovifanya wasanii wetu hapa nchini ambao ni kioo cha jamii...

Wiki kadhaa za nyuma iliwahi kushushiwa picha za fumanizi la msanii huyo dhidi ya msanii wake wa kike ambae alifumaniwa nae maeneo ya Kawe Jijini Dar ambapo sakata hili liliishia kituo cha Polisi Hananasifu baada ya msanii huyo kuridhia kumlipa mwenye mke kiasi cha shilingi laki tano.

Chanzo chetu kiliendelea kusema kuwa picha hizi za utupu zilipigwa siku nyingi kabla ya hilo fumanizi na zimevuja kutoka kwenye kamera yake mara baada ya kupotea ambapo blog hii ilifanya jitahada za kumtafuta msanii huyo kupitia simu yake ya kiganjani lakini kwa bahati mbaya hakuweza kupatikana.

Msanii huyo ambae sasa hivi ameachia filamu zake kama Bad Father,The,re ma sons, House Girl na Boss ambapo kati ya filamu hizo moja tu ndiyo iliyopelekwa kampuni ya Pilipili Entertainment ya Bad Father...

Bofya hapo chini kuziona picha hizo za uchi za msanii huyo chipukizi wa bongo movie....



WEMA SEPETU ASEMA..! "SITASAHAU KAMWE JINA ALILOKUWA AKINIITA BABA...."

Wema Isaac Sepetu ‘Madam’

WEMA Isaac Sepetu ‘Madam’ amefunguka kuwa kamwe hatasahau jina la Miss World ambalo marehemu baba yake, mzee Isaac Abraham Sepetu alikuwa akimuita.
Akizungumza na mwanahabari wetu wakati wa kuaga mwili wa baba yake nyumbani kwao, Sinza-Mori jijini Dar, Jumanne iliyopita, Wema alisema baba yake alikuwa akimuita jina hilo kama utani kutokana na masuala ya urembo aliyokuwa akiyafanya hivyo alipofariki dunia jina hilo ndiyo kumbukumbu yake ya muhimu.

Marehemu Isaac Abraham Sepetu.
“Sitalisahau jina la Miss World, baba ndiye alikuwa akiniita hivyo kila nilipokutana naye. Aliponiita hivyo nilikuwa nikifurahi sana,” alisema Madam.
Mwili wa baba Wema ulisafirishwa Jumatano (jana) kuelekea visiwani Zanzibar kwa ajili ya mazishi.

MAMA RWAKATARE ATENGWA NA MAKANISA KWASABABU YA ILE NDOA ALIYOFUNGISHA YA MBUNGE WA CCM ALIYEOLEWA NA KIJANA MDOGO...

 

MBUNGE wa Viti Maalumu, Mchungaji Getrude Rwakatare (CCM) wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Mikocheni B, jijini Dar es Salaam, ametengwa katika Ushirikiano wa Makanisa baada ya kanisa lake kulalamikiwa kufungisha ndoa inayodaiwa kukiuka taratibu za kikanisa, kisheria na kimaadili, Tanzania Daima Jumatano limejulishwa.Ndoa inayolalamikiwa kufungishwa na kanisa hilo ni ile iliyoibuliwa na gazeti hili wiki iliyopita ambayo inamhusisha Mbunge  wa Viti Maalumu, Rosweeter Kasikila (CCM) mwenye umri wa miaka 60 na kijana Michael Christian wa miaka  26.


Ndoa hiyo ambayo ilifungwa katika kanisa hilo Septemba Mosi mwaka 2011, imebaki kuwa gumzo na kuwaacha hoi baadhi ya mawaziri, wabunge pamoja na majirani wanaoishi jirani na mbunge huyo mjini Bagamoyo, Pwani.
 
Akizungumza na gazeti hili jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili na Haki za Jamii ya makanisa hayo, Mchungaji William Mwamalanga, alisema uamuzi wa kulitenga kanisa la Mama Rwakatare umetokana na kikao cha Kamati ya Maadili iliyokutana jana jijiji Dar es Salaam.
Alisema Kanisa la Mchungaji Rwakatare halifai kuendelea kuwa katika ushirika huo kutokana na kubariki ndoa hiyo aliyodai kuwa ni batili.
 
Mchungaji Mwamalanga alisema utaratibu wa ndoa katika makanisa unafahamika, ikiwa ni pamoja na wafungaji wa ndoa kutakiwa kutangaza ndoa hiyo hadharani kwa kipindi cha wiki tatu.
“Ndoa hii haikutangazwa hadharani, kibaya zaidi inasemekana imefungwa ndani ya ofisi na sio kanisani. Hiyo haiwezi kuitwaa ndoa maana haijakidhi vigezo na taratibu za kikanisa, ni lazima Mchungaji Rwakatare awajibike,” alisema.
 
Alisema lazima nyumba za ibada zikubali kutogeuzwa kichaka cha kusaidia uovu kama ilivyofanywa na kanisa hilo la Mikocheni B kwa kukubali kufanikisha ndoa hiyo kinyume cha taratibu.
“Tunalaani ndoa hiyo kuanzia mawio hadi machweo kwa kuwa hata maandiko ya kitabu kitakatifu cha Biblia kinawathamini yatima kama alivyo huyo kijana Michael anayeonekana kutoafiki ndoa hiyo kwa matakwa yake,” alisema mchungaji huyo.
 
Alisisitiza kuwa wanamtenga Mchungaji Rwakatare na kanisa lake kwani amewachafua  na kuyatia aibu makanisa mengine yote nchini.
 
Mchungaji huyo pia alimtaka Mwenyekiti wa CCM taifa, Rais Jakaya Kikwete kuwaengua kwenye chama hicho Mchungaji Rwakatare na Kasikila kuhusiana na ndoa hiyo.
“Rwakatare ni mtunga sheria, anajua wazi kuwa ndoa inatakiwa pia kubandikwa katika ubao wa matangazo. Ni wazi kuwa wameamua kuvunja sheria na kutenda kosa la jinai,” alidai.
 
Mwamalanga alisema kuwa kwa hatua hiyo ndoa hiyo ni batili na haramu kwa kuwa ni aibu pia kwa mtoto kumuoa mwanamke mwenye umri wa mama yake.
 
Katika hatua nyingine, mchungaji huyo alisema umoja wao unafanya kila iwezalo kuhakikisha kijana Michael anarudishiwa vyeti vyake ambavyo kwa sasa vimezuiliwa na Mbunge Kasikila.
Pia aliitaka Kamati ya Maadili ya Bunge kuwaita na kuwahoji wabunge hao kwa kitendo chao cha kuhalalisha ndoa hiyo kwani kimeutia doa muhimili huo.
 
Alisema Bunge ni sehemu tukufu, hivyo Rwakatare na Kasikila hawana hadhi ya kukaa huko, hivyo alishauri waenguliwe.
 
Alipopigiwa simu kueleza msimamo wake juu ya uamuzi wa umoja wa makanisa hayo kumtenga kwa kuhalalisha ndoa hiyo, Mchungaji Rwakatare aling’aka na kukata simu.
Alipopigiwa tena simu yake ilizimwa na hakuweza kupatikana tena hadi tunaenda mitamboni.
  

- Tanzania Daima

HATIMAYE UVUMILIVU WAMSHINDA IRENE UWOYA NA KUANZA KUSHUSHA MATUSI MTANDAONI ...KISA BOFYA HAPA

“...Wale ma-(Tusi linalohusisha kiungo cha mwili) wanao post (Tusi kama la hapo mwanzo) humu...waaandike watakavyo...sio (Tusi- vitendo vibaya kwenye jamii) tuuu yan na vza yakuzunguka dunia nzima....siitaj watu ma-(Tusi kali sana)...kama na kuboa kafe mbele....eti range nimehongwa mtasubiri sanaaaa....sina mdaa huo sinaaa...wakukaa pemben na kumsmanga mtuuuu...wote mnao ni disss ma-(Tusi la kumalizia sentensi)...
Hayo ni maneno ya mwadada Irene Uwoya aliyoaandika usiku wa leo hii kupitia ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii. Tulipoyasoma tuu, tulishtushwa sana kwani si kawaida kwa mwanadada huyu kuandika maneno mzito kama haya na ndipo tulipoamua kufanya utafiti yakinifu ili tujue why??? Na haya ndo majibu ya uchunguzi wetu huu…
Tujikumbushe Historia fupi
Hivi majuzi mwadada Irene Uwoya alipost kwenye mtandao picha za gari yake mpya aina ya Range Rover na ndipo watu wengi walianza ku-comment na “kumponda” mwanadada huyu kuwa sio yake bali kahongwa na wanaume “wanaomuweka mjini”
Irene akajibu
Siku si nyingi baadae Irene aliwajibu kwa kusema kuwa gari hiyo ni yake na wote wanaosema kahongwa watasubiri sana maana hiyo ni matokeo ya jasho lake
Msiba wa baba yake wema wahusishwa
Kwa bahati mbaya mwanadada Wema Sepetu alipata matatizo ya kufiwa na baba yakehivi majuzi na ndipo zikatoka tetesi kuwa ETI mwanadada Irene pamoja na kundi jingine la mastaa Fulani wamesusa kuhudhuria msiba huo kwa madai kuwa Wema huwa hashiriki misiba ya wengine
Mashabiki wa wema wamjia juu
Baada ya mambo hayo yote hapo juu ndipo kundi la mashabiki wa wema walipoanza kuandika kwenye ukurasa wa mwanadada huyo, wakimutukana na kumponda sana eti hilo gari sio lake bali kahongwa na jamaa mmoja hivi (Jina tunalihifadhi kwa sababu za kiusalama) na hivyo asiwadanganye wananchi mambo ambayo si kweli
Uvumilivu ukawa mchache kwa Irene
Baada ya matusi na maneno mengi ya kejeli toka kwa mashabiki hao kumzidi Irene hatimaye ndio ameamua kuandika hayo hapo unayoyaona juu. Daah, hatari sana mjini hapa ukiwa staa.

Tanzania yamzuia Benard Membe kuhudhuria vikao vya jumuiya ya Afrika Mashariki....Waziri Siita atoa wiki mbili za kuitema jumuiya hiyo



SERIKALI iko katika mazungumzo na nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Burundi ili kushirikiana kwa baadhi ya maeneo, hasa kutokana na ukweli kuwa baadhi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Rwanda, Kenya na Uganda, zimeonesha mwelekeo wa kujitenga.
 
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, alisema hayo jana alipokuwa akitii mwito wa Spika, Anne Makinda, kujibu maswali ya wabunge, waliokuwa wakihoji kwa nini Tanzania nayo isijitenge.
 
“Kiuchumi sisi ni majirani zaidi na DRC… Rwanda inaangalia barabara tunayoshirikiana kuijenga kufika Burundi, ila ujenzi wa reli ya Uvinza-Msongati itaokoa wenzetu wa Burundi, kwani wakitumia bandari ya Mombasa kwenda Bujumbura, kwao ni mbali kwa zaidi ya kilometa 900, tofauti na Dar es Salaam kwenda Bujumbura,” alifafanua Sitta.
 
Kabla ya kutoa ufafanuzi huo, wabunge walitaka Serikali isikubali kuchezewa na baadhi ya nchi za EAC na kuitaka ijitoe mara moja na ikiwezekana, iunde Jumuiya yake ikishirikisha Burundi na DRC.
 
Aliyeibua suala hilo la kutaka Tanzania ijitenge ni Mbunge wa Viti Maalumu, Rukia Ahmed (CUF), ambaye katika swali lake la nyongeza aliitaka Serikali ieleze inasubiri nini kujitoa katika Jumuiya hiyo kutokana na kuendelea kutengwa na marais wa Rwanda, Kenya na Uganda ambao wamekuwa wakikutana bila Tanzania na wanajumuiya wengine kushirikishwa.
 
Pia, alitaka nchi ijitoe kwa kutumia Ibara ya 145 ya Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya hiyo na kunukuu kauli ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kuwa Tanzania inasubiri talaka kutoka jumuiya hiyo.
 
Mbali na swali hilo la nyongeza, katika swali la msingi, Mbunge wa Mbinga Magharibi, John Komba (CCM), alisema kabla ya Rwanda na Burundi kujiunga na EAC, hali ilikuwa tulivu na yenye maelewano makubwa.
 
Aliongeza kuwa baada ya nchi hizo kujiunga na Jumuiya, sasa hali ni tete na kuhoji ni kitu gani kilisababisha nchi hizo kujiunga na Jumuiya na kwa nini Tanzania isijitoe kama ilivyofanya kwenye Soko la Pamoja la Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA).
 
Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango-Malecela (CCM), alitaka Tanzania isitishe kushiriki shughuli zote za Jumuiya kwa kile alichosema inaelekea kufa. Kutokana na uzito wa suala hilo, Spika wa Bunge, Makinda alimtaka Waziri Sitta, kujibu maswali hayo kwa pamoja. Kero, kususa Sitta alisema ni kweli inakera kuona wanajumuiya wengine wanaizunguka Tanzania na kusema hawajakaa kimya katika kushughulikia suala hilo.
  
Alisema kwa sasa mambo yote yanayohusu Jumuiya, ambayo baadhi ya nchi wanachama wamekutana kwa siri na kuyatolea msimamo na kuja nayo katika mikutano ya pamoja, Tanzania haitashiriki. Alitoa mfano wa mambo yanayohusu sera za mambo ya nje, ambapo alisema yeye hatashiriki vikao vyote, ambavyo wanajumuiya wengine tayari wana msimamo.
 
“Kesho (leo), Burundi kuna mkutano, nimemwambia Naibu Waziri asihudhurie, Katibu Mkuu wa Wizara atakwenda lakini hatatoa msimamo wowote wa Serikali, maana si kazi yake, bali yetu sisi wanasiasa,” alisema Sitta.
 
“Tulishamhoji Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa EAC kuhusu hili, kama tutaendelea na uongo wa kitoto tutakuja bungeni, kwenu waheshimiwa wabunge na kumaliza hili, hatutakubali liendelee, lakini kwa sasa tufuatilie mpaka mwongo aumbuke,” alisema Sitta.
 
Alisisitiza kwamba huu ni wakati wa kufuata ushauri wa Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, aliyepata kusema “Mtu mwongo mwongoze”, na kuongeza kuwa kama wana Jumuiya wengine wana hila, itajulikana tu, kwa kuwa hata juzi walikutana Kigali, Rwanda bila kushirikisha Tanzania. Sitta alisema baada ya wiki mbili, majibu ya Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo, yatatolewa na hapo nchi itatoa uamuzi.
 
Akijibu swali la nyongeza la Komba, aliyetaka kujua kwa nini Jumuiya hailaani vitendo vya kuunda Jumuiya mpya ndani ya nyingine na kuitaka Tanzania iunde Jumuiya yake na DRC na Burundi, na swali la Ahmed aliyetaka Tanzania isisubiri talaka kujitoa, Sitta alisema haijaanzishwa Jumuiya nyingine, ila wapo katika harakati fulani.
 
Kuhusu kutosubiri talaka, Sitta alisema asilimia 52 ya eneo la Afrika Mashariki, linaundwa na Tanzania huku asilimia 48 ikichukuliwa na nchi nyingine, hivyo suala la nani anatoa talaka, lina uzito kwetu zaidi na kuongeza kuwa, kama ni nani mwoaji, Tanzania ndiyo imeoa na labda ndiyo itoe takala na si kupewa.
 
Msimamo Sitta akijibu swali la Msingi la Ahmed, aliyetaka kujua msimamo wa Serikali wa mambo yanayohusu Jumuiya hasa kutokana na mkutano uliofanyika Mombasa siku ya ufunguzi wa bandari hiyo, kujadili pamoja na mambo mengine, masuala ya biashara, miundombinu na Shirikisho la Afrika Mashakiri, alisema mikutano ya wakuu wa Kenya, Rwanda na Uganda bila kuishirikisha Tanzania, ilianza Entebbe, Uganda Juni 24 na 25.
 
Alisema mkutano wa pili ulifanyika Mombasa Agosti 28 kwa kigezo cha uzinduzi rasmi wa gati namba 19, ambayo imepangwa mahususi kushughulikia mizigo ya Rwanda na Uganda.
 
"Pamoja na suala hilo la bandari ya Mombasa, ilijitokeza kwamba wakuu hao wa nchi tatu walijadili pia masuala ya uanzishwaji wa Himaya Moja ya Forodha, uanzishwaji wa hati moja ya kuishi katika nchi hizo (viza) kwa watalii, matumizi ya vitambulisho vya Taifa kwa nchi zao na harakati za Shirikisho la Kisiasa la nchi zao.
 
“Kwa kuzingatia kuwa masuala hayo yapo katika hatua mbalimbali za majadiliano katika Jumuiya na nchi zote tano hushiriki, Tanzania katika mkutano wa 27 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya uliofanyika Arusha Agosti 31, tulidai ufafanuzi," alisema Sitta.
 
Alisema walimtaka Mwenyekiti wa Baraza kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu mikutano hiyo ya utatu inayoendeshwa sambamba na mikutano ya kawaida ya kalenda za Jumuiya na kwamba kikao cha Baraza hilo cha kutathmini hali hiyo, kinatarajiwa kufanyika wiki ya pili ya mwezi ujao Arusha.
 
Sitta alisisitiza wakati taarifa hiyo ikisubiriwa, msimamo wa Tanzania ni kuwa masuala yote yanayojadiliwa na kuamuliwa nje ya utaratibu wa Jumuiya, haitayatambua kama uamuzi wa Jumuiya na utekelezaji wake utahusu nchi husika pekee.
Kifo kujirudia? Iwapo sintofahamu hii itaendelea kama ilivyo na hata kufikia hatua ya Tanzania kujitoa, EAC itakuwa inasambaratika kwa mara nyingine, baada ya kutokea hivyo mwaka 1977.
Tukio la mwaka 1977 lilitokana na nchi tatu wanachama wakati huo, Tanzania, Kenya na Uganda, kutofautiana kisiasa huku Tanzania na Uganda zikiwa katika uhusiano mchungu uliosababisha vita baina yao.
 
Wakati Jumuiya ya kwanza ikivunjika, nchi hizi zilikuwa zikiongozwa na Mwalimu Julius Nyerere wa Tanzania, Mzee Jomo Kenyatta wa Kenya na Dk Milton Obote wa Uganda, ambao wote sasa ni marehemu.
 
Novemba 30, 2001 Jumuiya ilifufuliwa chini ya marais Mwinyi (Tanzania), Daniel arap Moi (Kenya) na Yoweri Museveni wa Uganda katika sherehe zilizofanyika Arusha.
 
Rwanda na Burundi zilijiunga rasmi na Jumuiya hiyo Juni 18, 2007 katika mkutano wa marais wa EAC jijini Kampala, Uganda, na kushuhudiwa na marais Mwai Kibaki (Kenya), Museveni, Jakaya Kikwete (Tanzania), Paul Kagame (Rwanda) na Pierre Nkurunziza (Burundi).

Tazama  video  ya  majibu  ya  waziri  Sitta
 
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger