Sanamu
kubwa zaidi duniani ya Nelson Mandela imezinduliwa katika mji mkuu wa
Afrika kusini Pretoria siku moja baada ya rais huyo wa zamani kuzikwa
.
Sanamu
hiyo iliyotengenezwa kwa shaba ina urefu wa mita tisa na ina uzani wa
tani nne unusu. Ilizinduliwa katika bustani la majengo ya bunge na
inaonyesha Nelson Mandela akihimiza umoja na maridhiano.
Sanamu hiyo yenye mikono ya Mandela ikiwa wazi ilinuiwa kuonyesha Mandela alivyoliungaisha taifa zima kwa mapenzi yake
.
Bwana Mandela lipewa mazishi ya kitaifa nyumbani alikozaliwa katika kijiji cha Qunu Jumapili
Familia
ya Madiba , viongozi wa ANC , viongozi wa Afrika na maafisa wengine
wakuu walihudhuria mazishi hayo katika kijiji cha Qunu mkoani Cape
Mashariki
.
Kifo
cha Mandela kilifuatwa na maombolezi ya siku kumi na sherehe za
kukumbuka maisha ya Mandela aliyefariki akiwa na umri wa miaka 95
.
Bendera ya nchi hiyo ilirejeshwa kupepea katika urefu wake wa kaiwada.
Mandela
anakumbukwa kwa juhudi zake za kupatanisha wananchi na kupigia debe
msamaha miongoni mwa watu na ndio maana leo ikawa siku iliyotengwa kwa
ajili ya uzinduzi wa sanamu hiyo
.
Wakati
wa utawala wa wazungu, terehe 16 Disemba ilijulikana kama siku ya
kuwakumbuka mashujaa wa Afrikaners walioshinda vita dhidi ya jeshi la
Zulu mwaka 1883.
Zaidi ya karne moja baadaye mwaka 1961, Mandela alizindua jeshi lake la Umkhonto we Sizwe kupigana dhidi ya utawala wa wazungu
BBC.