Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juzi lilisitisha shughuli zake na kutoa Azimio kutokana na kifo cha Mandela, kwa kumuenzi kwa kudumisha umoja, amani, mshikamano ili kuleta maendeleo.
Wakichangia
Azimio hilo, wabunge wametaka kutokana na kifo cha mpigania uhuru huyo
kujifunza kwa kutolipiza kisasi kwa kusameheana na kuvumiliana katika
kila jambo, hususan suala la Katiba na mijadala mbalimbali.
Awali,
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Edward Lowassa
aliwasilisha azimio hilo la kuungana na nchi ya Afrika Kusini,
kuomboleza kifo cha muasisi, mpinga ubaguzi wa rangi na Rais wa Kwanza
mweusi wa Afrika Kusini.
Alisema,
“Mandela aliyatoa maisha yake kupigania uhuru wa Waafrika na kupinga
ubaguzi wa rangi uliokuwa ukiendeshwa na utawala wa wazungu wachache
nchini Afrika Kusini, hali iliyofanya kufungwa katika Gereza la Robben
tangu mwaka 1964”.
Mandela
alizaliwa mwaka 1918 na kufungwa kwa miaka 27. Baada ya kutangazwa kuwa
Rais wa nchi hiyo mwaka 1990, alionesha ukomavu wa uongozi kwa kusamehe
wote waliomtesa gerezani na kuwaunganisha watu wa nchi hiyo weusi na
weupe.
Mwaka
1999 alistaafu mwenyewe urais na kurithisha madaraka kidemokrasia hivyo
kwa azimio hilo Bunge litamuenzi kwa utu na kuthamini wengine.
Alisema
Bunge linaazimia kuungana na familia yake, wananchi wa Afrika Kusini na
dunia nzima katika kuomboleza msiba wa Nelson Mandela, kwani amekufa,
lakini ataendelea kuishi katika mioyo yetu kwa miaka mingi.
Wakichangia
na kuunga mkono azimio hilo lililopitishwa na Spika wa Bunge, Anne
Makinda ambaye alitangaza kulipeleka katika Bunge la nchini Afrika
Kusini, wabunge waliungana katika kuomboleza na kusema bara limepoteza
mtu muhimu.
Mbunge
wa Jimbo la Mkanyageni, Habibu Mnyaa (CUF) alisema kifo cha Mandela
kimeunganisha watu wa mataifa yote duniani, hasa waliochukia
unyanyasaji, bila kujali wapo umbali gani.
“Hata
baada ya kifo pia ameunganisha dunia kwa nchi zote hata zenye mitazamo
tofauti kupeperusha bendera nusu mlingoti na kuungana kuomboleza,”
alisema Mnyaa.
-Habari leo.
-Habari leo.