UCHAFU unaendelea kufichuliwa! Safari hii Oparesheni Fichua Maovu (OFM) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Wilaya ya Temeke wamekifyeka kichaka cha ngono maeneo ya Mbagala-Zakhem jijini Dar, Risasi Jumamosi linakupa habari kamili.
Tukio hilo limetokea juzikati usiku wa manane baada ya wakazi wa kitongoji hicho kuchoshwa na tabia za madadapoa hao waliokuwa wakifanya vitendo vichafu karibu na nyumba zao na kutoa taarifa kwa OFM.
Kikosi hicho kiliwasiliana na Kamanda wa Polisi Kanda ya Temeke, Englebert Kiondo na kupewa askari wa Kituo cha Mbagala Kizuiani na kwenda kukifyekelea mbali kichaka hicho.
Kondom zikiwa zimezagaa eneo la tukio. |
Walionaswa wakiwa katika difenda. |
Pia, kikosi hicho kilimkuta mteja mmoja akiwa anapewa huduma hiyo ndani ya kichaka hicho kilichotapakaa kila aina ya kondom katika kona zote.
Ndani ya kichaka hicho, kulikuwa na sehemu maalum ya kufanyia ngono ambayo ilikuwa imetandikwa boksi chafu huku sehemu ya mlango ikizibwa na gunia aina ya ‘salfeti’.
OFM ilibaini kwamba kabla ya dadapoa na mteja wake kuingia ndani ya kichaka hicho, kulikuwa na malipo ya fedha kwa mmiliki wa kichaka hicho ambaye alifahamika kwa jina maarufu la Babu ambaye hata hivyo, alifanikiwa kukimbia baada ya kuona madadapoa hao wakikamatwa.
Pamoja na hayo, oparesheni hiyo ilimnasa kahaba mdogo kuliko wote aliyejitambulisha kwa jina moja la Sarah (16) ambaye alidai kuwa ni yatima kutoka Mkoa wa Mtwara na alijichanganya katika biashara hiyo haramu kwa ajili ya kutafuta kipato kwa kuwa hana ndugu wa kumsaidia.
Oparesheni hiyo pia ilimnasa mama mtu mzima aliyejitambulisha kwa jina moja la Joyce (38).
Pamoja na mama huyo kuhojiwa sababu ya kuingia katika biashara hiyo aligoma kuzungumzia kutokana na aibu.
Watuhumiwa wengine pia waligoma kutoa ushirikiano kwa OFM kwa kuhofia kuvunja ndoa zao kwa kuwa ilibainika kwamba wengi wao ni wake za watu.
Madadapoa hao pamoja na mteja aliyenaswa walipelekwa katika Kituo cha Polisi cha Kizuiani na kufunguliwa jalada la kesi namba MBG/RB/11343/13 KUFANYA VITENDO VYA UMALAYA, kabla ya kupandishwa kizimbani kwa hatua zaidi za kisheria.