Kanali
Makenga alizoea kutembea na bakora, ishara kuwa alikuwa mfugaji na pia
kamanda wa kijeshi aliyetaka majeshi yake kuwa na nidhamu na kumtii.
Mrefu
na mwembamba , Makenga alikulia katika maeneo ya milimani mkoani Kivu
Kusini ndani ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, na alisifika sana kwa
kuwa mlenga shabaha na mtu mwenye maarifa na mwenye ujuzi wa kupanga
mambo ya kijeshi.
Alipata
ujuzi wake wa kijeshi nchini Rwanda, ambako alikuwa mmoja wa wapiganaji
wa Rais Paul Kagame kabla ya kuchukua mamlaka mjini Kigali.
Baadaye
alirejea DR Congo na kuwa mtu mashuhuri katika harakati za kudai haki
za wenyeji wa Tutsi wa Congo ambao pia ni wachache.
Maisha ya Kanali Makenga kama mwanajeshi yalifana sana wakati wanajeshi wa M23 walipoteka mji wa Goma , Mashariki mwa DR Congo.
Pia alimshinda hasimu wake wa kijeshi ndani ya M23 Kanali Bosco Ntaganda – na kumwondoa kama kamanda wa wapiganaji wa M23.
Ntaganda alikimbilia nchini Rwanda ambako alijisalimisha kwa ubalozi wa Marekani.
Sasa yuko katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC, akisubiri kufunguliwa mashitaka ya uhalifu wa kivita.
Ikiwa hatafanikiwa kukubaliana na serikali ya DRC, Makenga huenda na yeye pia akafikishwa ICC.
Ingawa
hakuna kibali cha kumkamata, baraza la usalama la Umoja wa Mataifa
lilimwekea vikwazo vya usafiri pamoja na kupiga tanji mali zake, mwaka
jana likimtuhumu kwa kuongoza uasi wa M23 na kuwafanyia ukatili raia wa
Congo, Mashariki mwa nchi.
Lakini kulingana na kanali Makenga, alipigana vita halali akitetea haki za jamii ya watutsi.
Mwaka
huu wote kumekuwa na tetesi kua yuko katika hili mbaya ya kiafya na
kujisalimisha kwake ni ishara kuwa huenda asirejee tena vitani.