MZEE mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Abdullahimu Mnami (48) amenaswa akiendesha gesti bubu kinyume cha sheria za nchi.
Baadhi ya wananchi walionaswa katika msako wa biashara haramu ya ukahaba. Pichani ni wauzaji na wanunuzi.
Tukio hilo lilitokea Oktoba 26, mwaka huu maeneo ya Tuangoma jijini
Dar, baada ya waandishi wetu kuzinyaka taarifa hizo na kuzifikisha kwa
mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo, Chande Mohammed aliyefika eneo hilo
na polisi.Awali, ili kujiridhisha, mmoja wa mapaparazi wetu alijifanya mteja na kufika katika gesti bubu hiyo, kisha kupangisha chumba kwa malazi ya siku moja kwa malipo ya shilingi 3000 tu lakini pasipo kuandikisha mahali popote.
Mmiliki wa gesti bubu inayotumika katika biashara haramu ya ukahaba baada ya kutiwa nguvuni.
Akizungumza na waandishi wetu mbele ya maaskari na mwenyekiti, mzee
huyo alisema alishindwa kuisajili gesti yake kwa kuwa haikuwa na viwango
vinavyokubalika na manispaa (ya Temeke).“Ningefuata utaratibu, manispaa isingeniruhusu kutokana na ubora wa vyumba vyenyewe, kama mnavyoona. Pia njaa tu jamani ndiyo imenifanya nianzishe gesti hii,” alisema mzee Abdullahim.
Eneo la ndani ya gesti bubu inayotumika kwa ukahaba.
Hata hivyo mwenyekiti wa mtaa huo, alisema kuwa mzee huyo ana kesi ya
kujibu kwa kukiuka taratibu za kibiashara zilizowekwa na halmashauri na
kumuamuru aifunge gesti hiyo mara moja huku akiahidi kumpeleka Baraza
la Kata kwa ajili ya masikilizano ya awali.Timu yetu iliwaachia msala wao na kuendelea na oparesheni nyingine ambapo walifanikiwa kuwanasa machungudoa wakijiuza jirani na mtaa huo huku ikielezwa kuwa, wateja wa madadapoa hao hupelekwa katika gesti bubu ya mzee huyo kwa vile ni bei poa.
Wateja na wafanyabiashara haramu ya ukahaba wakiwa chini ya ulinzi baada ya kunaswa.