Mtuhumiwa namba 8 katika kesi ya mauaji ya Mfanyabiashara wa Madini ya
Tanzanite Erasto Msuya, aliyekamatwa hivi karibuni Ally Musa "Majeshi"
akipelekwa katika chumba cha mahakama ya hakimu mkazi mjini Moshi kwa
ajili ya kuunganishwa na watuhumiwa wenzake katika kesi hiyo.
Mtuhumiwa namba mbili,
Shaibu Shaibu Jumanne Saidi maarufu kama Mredi(38) anayetuhumiwa
kushiriki Mauaji ya mfanyabiashara wa madini Erasto Msuya wakipelekwa
katika jengo la mahakama.
Mmoja wa askari akijaribu kutoa maelekezo kwa mtuhumiwa wa mauaji ya
mfanyabiashara wa madini Erasto Msuya wakati akielekea chumba cha
mahakama ya hakimu mkazi mjini Moshi.
Ndugu wa marehemu Erasto Msuya wakiwa nje ya jengo la mahakama ya
Watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya mfanyabiashara wa madini Erasto Msuya
wakitolewa katika chumba cha mahakama mara baada ya kuahirishwa kwa
shitaka linalo wakabili.
Watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya mfanyabiashara wa madini Erasto Msuya
wakitolewa katika chumba cha mahakama mara baada ya kuahirishwa kwa
shitaka linalo wakabili.
Mtuhumiwa namba mbili,
Shaibu Shaibu Jumanne Saidi maarufu kama Mredi (38) anayetuhumiwa
kushiriki Mauaji ya mfanyabiashara wa madini Erasto Msuya, akisaidiwa
kupanda katika gari mara bada ya kuahirishwa kwa shitaka linalo
wakabili.
MTUHUMIWA “Muhimu”
katika kesi ya mauaji ya Bilionea wa madini ya Tanzanite, Erasto Msuya
(43), Ally Mussa “Majeshi” (42) amepandishwa mahakamani LEO katika
Mahakama ya hakimu mkazi Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Mtuhumiwa huyo
aliyekamatwa Oktoba 8, mwaka huu, alinaswa mkoani Kigoma akijaribu
kutorokea nchini Burundi baada ya kufanikiwa kukimbia mitego ya polisi
katika mikoa ya Arusha, Dodoma na Mwanza na kurudishwa mkoani
kilimanjaro ambapo jana aliunganishwa katika kesi ya Mauaji ya Msuya.
Akisoma Mashtaka
yanayomkabili Mtuhumiwa huyo mbele ya Mahakama ya Hakimu Munga Sabuni,
Mwendesha Mashtaka, Wakili wa Serikali, Janet Sekule alisema Mshtakiwa
huyo pamoja na wenzake Saba, wanashtakiwa kwa kosa la kuua kwa kukusudia
kinyume cha kinyume cha kanuni namba 16,kifungu cha 196 ya sheria za
makosa ya jinai, “Kinyume cha sheria ya makosa ya jinai, kanuni ya 16,
kifungu cha 196, Ally Mussa au kwa jina lingine Majeshi, walimuua Erasto
Msuya katika maeneo ya Mjohoroni, njia panda ya Arusha na KIA kwa
kumpiga risasi,” alisema Sekule.
Aidha baada ya kusoma
maelezo ya shtaka hilo, upande wa Jamhuri, ukiwakilishwa na Wakili wa
Serikali, Janet Sekule iliiomba Mahakama ya Hakimu Sabuni kuipa muda
kuweza kukamilisha upelelezi ambapo kesi hiyo iliahirishwa hadi Oktoba
28, mwaka huu, itakapo tajwa tena.
Ally Mussa “Majeshi”,
anayedaiwa kuwahi kulitumikia Jeshi la kujenga Taifa (JKT), kabla ya
kufukuzwa anaungana na Sharif Mohamed Athuman (31) mchimbaji mdogo wa
madini na mkazi wa Kimandolu mkoani Arusha, Shaibu Jumanne Saidi maarufu
kama Mredi (38), mkazi wa Songambele Wilaya ya Simanjiro.
Wengine ni Joseph Damas
Mwakipesile maarufu kama Chusa (36), mfanyabiashara wa madini na mkazi
wa Arusha, Jalila Zuberi Said (28), mkazi wa Babati, Sadiki Mohammed
Jabir ‘Msudani’ au ‘Mnubi’(32), mkazi wa Dar es Salaam na Lang’ata
wilayani Hai na Karim Kihundwa (33) mkazi wa Kijiji cha Lawate Wilaya ya
Siha na Mussa Juma Mangu (30), mkazi wa Shangarai kwa Mrefu mkoani
Arusha.
Hata hivyo Mwandishi wa
Habari hizi alishuhudia kesi hiyo ikisomwa katika hali ya utulivu
tofauti na ilivyozoeleka kwani katika mara zote kesi hiyo ilipofikishwa
Mahakamani hapo kulikuwa na umati mkubwa wa watu wakiwemo ndugu za
Marehemu Erasto Msuya.
Mfanyabiashara Erasto
Msuya, aliuawa Agosti 7, mwaka huu majira ya 6:30 mchana kwa kupigwa
risasi 13 kifuani, kando ya barabara kuu ya Arusha– Moshi katika eneo la
Mjohoroni, Wilaya ya Hai, karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Kilimanjaro (KIA).
Credit: kijiwe