Wakati Rais Jakaya Kikwete akituma
salamu za rambirambi kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Bernard Membe kutokana na kifo cha Balozi Isack Sepetu, mke
wa marehemu amelaumu baadhi ya viongozi wa Serikali, akidai
walimtelekeza mumewe kwa kushindwa kushiriki kumuuguza badala yake
kuachia familia pekee.
Mariam, ambaye ni mke wa pili wa Balozi
Sepetu aliyefunga naye ndoa ya kimila mwaka 1982, alisema mumewe enzi
za uhai wake aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi, ikiwamo ya
Ubalozi Urusi na kwamba, kwa kutambua mchango wake, Rais wa Zanzibar, Dk
Ali Mohamed Shein aliagiza agharimiwe matibabu lakini hakuna hatua
zilizochukuliwa.
Akizungumza jana nyumbani kwake, Sinza
Dar es Salaam, Mariam alisema alijaribu kuwasiliana na Wizara ya Afya
Zanzibar, lakini hakupata ushirikiano aliopata, aliamua kumsafirisha
mumewe huyo kutoka Zanzibar hadi Dar es Salaam Oktoba 24, mwaka huu na
kumpeleka Hospitali ya TMJ Mikocheni.
“Nishukuru
watoto wake wote waliungana na kushiriki kikamilifu kumuuguza baba
yao, wakishirikiana na ndugu na jamaa zetu wachache. Kwa kweli jambo
hili limenihuzunisha sana nafikiri hakupata huduma ya kutosha,” alisema