KOCHA wa Galatasaray, Roberto Mancini
anapanga kumchukua winga wa wapinzani wake wa zamani katika Jiji la
Manchester, Antonio Valencia wa United.
Kocha huyo wa zamani wa Manchester City
anamataka mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ecuador kwa dau la Pauni
Milioni 12.5 ili kuimarisha alichokirithi kwa Fatih Terim.
Kocha wa Old Trafford, David Moyes
amemuondoa Valencia katika orodha ya wachezaji muhimu, na kuibuka kwa
nyota kinda, Adnan Januzaj kumempunguzia nafasi katika kikosi cha
kwanza.
Mwanzo mpya: Kocha wa Galatasaray, Roberto Mancini anataka kumsajili winga wa Manchester United, Antonio Valencia
Anapambana kuwa fiti: Valencia, (kushoto)
akiwa mazoezini na timu ya taifa ya Ecuador wiki hii, amepoteza nafasi
kikosi cha kwanza cha United
Shetani Mwekundu: Valencia (kushoto)
alisajiliwa United mwaka 2009 kutoka Wigan, lakini sasa anaweza akawa
anachungulia mlango wa kutokea
Na sasa Valencia anaweza kupata nafasi Galatasaray, kwa mujibu wa gazeti la Uturuki, Fanatik.
Pamoja na hayo wanaweza kukabiliana na
upinzani kutoka klabu ya zamani wa Moyes, Everton, ambayo inamtaka winga
huyo kama sehemu ya dili ya kumuuza Leighton Baines Januari.
Dili litamaanisha kwamba Mancini
atatakiwa kupunguza mchezaji wake mmoja wa kigeni katika kikosi cha sasa
ili kuendana na sheria ya idadi ya wachezaji wa kigeni ya Shirikisho la
Soka Uturuki.
Mshambuliaji wa zamani Chelsea, Didier
Drogba kwa sasa anaongoza safu ya ushambuliaji ya timu hiyo ya Uturuki,
na Mancini anataka kuweka alama yake katika kikosi hicho.
Everton inaweza kumtaka Valencia katika mauzo ya Leighton Baines,aliye mazoezini na kikosi cha England training
Winga teleza: Nafasi ya Valencia katika kikosi cha kwanza United imepungua baada ya kuibuka kwa Adnan Januzaj