Mac
Elvis alikuja Tanzania wiki mbili zilizopita kwa ajili ya consert Dar
es salaam akiwa na wasanii wenzake kutoka Uganda ambao walirudi baada ya
consert ila yeye akabaki ili kufanya kolabo na baadhi ya wasanii wa
Tanzania.
Mtanzania Gee ambae ni rafiki yake,
anasema ‘Alhamisi Elvis alikwenda kumtembelea rafiki yetu mmoja anaitwa
Lulu (Sio mwigizaji) anaishi Mbezi Beach Africana ambapo Ijumaa jioni
mida ya saa moja alijisikia kwenda kuogelea kwenye swimming pool, Lulu
alimwambia asiogelee kwa sababu ilikua usiku umeshaingia lakini Elvis
aliiamua kuogelea hivyohivyo’
‘Lulu alitoka nyumbani kidogo wakati
huo Mac akienda kuogelea akiwa mwenyewe, ilikua ni kawaida kwake
kuogelea mara nyingi huwa anapenda kuogelea hivyo hakikua kitu kigeni…
Lulu aliporudi hakumuona Mac manake hakurudi hivyo akadhani mwimbaji
huyu ameshaondoka, akawa anampigia simu rafiki anaeishi na Mac lakini
haikupokelewa’ – Gee
‘Kesho
yake mida ya saa nne mlinzi ndio akaona nguo pembeni na aliposogelea
akaona mwili wa Mac ndani ya swimming pool chini ambapo baada ya
kutolewa alionekana akiwa na jeraha kwenye paji la uso hivyo inaonekana
alijigonga akitaka kujirusha, tumbo lake halikujaa maji kama ambavyo
ilidhaniwa, tayari mipango ya kumsafirisha imekamilika na anapelekwa
kwao Uganda leo October 22 2013′ – Gee