MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora imewahukumu adhabu ya kunyongwa hadi kufa washitakiwa sita, baada ya kupatikana na hatia ya kuua kwa kukusudia. Imetoa adhabu hiyo katika kikao chake kinachoendelea mkoani Shinyanga.
Adhabu hiyo ilitolewa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora, Simon Lukelelwa katika kesi nne tofauti. Kesi hizo ni za mauaji ya kikatili dhidi ya wanawake vikongwe, kutokana na imani potofu za kishirikina.
Mauaji hayo yalifanyika kati ya mwaka 2005 na 2007 katika Wilaya za Bukombe, Shinyanga na Kahama, ambako wanawake wanne waliuawa kikatili kwa kukatwa mapanga sehemu mbalimbali za miili.
Waliopewa adhabu hiyo ni Venance Nuba na Tegemeo Paulo, ambao walitiwa hatiani kwa kosa la kumuua kwa kukusudia Sophia Gundu Januari 25,2006 katika Kijiji cha Kazibizyo Wilaya ya Bukombe Mkoa wa Geita.
Wengine wawili waliokumbwa na adhabu ya kifo cha kunyongwa ni Joseph Lushika na Maziku Mpiga Chai baada ya kupatikana na hatia ya kumuua kwa kukusudia Monica Bulemela Mei 5, 2005 katika Kijiji cha Lutembela Wilaya ya Bukombe.
Mshitakiwa mwingine aliyekumbwa na adhabu ya kunyongwa ni Mhande Manyanya baada ya kupatikana na hatia ya kumuua kwa kukusudia Wande Bulugu Julai Mosi, 2007 katika Kijiji cha Ihapa Wilaya ya Shinyanga mkoani hapa.
Mshitakiwa wa sita aliyekumbwa na adhabu ya kunyongwa baada ya kupatikana na hatia ya kuua kwa kukusudia ni Tembo Hussein, aliyetiwa hatiani kumuua kwa kukusudia Anjelina Hungwi katika kijiji cha Itega Wilaya ya