KARIBU
katika mechi ya gharama kubwa zaidi duniani – wachezaji 22 wa bei mbaya
zaidi daima wenye thamani ya Pauni Milioni 417 kuumana uwanjani...
Barcelona wanaikaribisha Real Madrid leo Jumamosi katika El Clasico ya
kwanza msimu huu: Messi v Ronaldo, Neymar v Bale, Pique v Ramos.
Huku
timu ya Carlo Ancelotti ikizidiwa pointi tatu na kikosi cha Gerardo
Martino katika La Liga, kipigo kitatengeneza tofauti kubwa baina ya timu
hizo mwanzoni mwa msimu.
Katika miaka ya karibuni imekuwa mechi ya mchuano mkali, ufundi, na mabao.
Wanawafukuzia: Real wapo nafasi ya tatu, wakiwa wameshinda mechi saba, sare moja na kufungwa moja katika mechi tisa
Barcelona (4-1-2-3)
Victor Valdes – Akademi
Alitarajiwa
kuondoka Nou Camp msimu huu bada ya Monaco kutoa ofa kubwa ya kumnunua
na Pepe Reina akatajwa kuja kuziba pengo lake, lakini kipa huyo mwenye
umri wa miaka 31 amebaki na amedaka mechi saba bila kuruhusu nyavu zake
kutikiswa msimu huu katika mechi 12. 7/10.
Namba 1: Valdes (kushoto) ni kipa anayeheshimika Ulaya
Dani Alves - Pauni Milioni 23
Bila
shaka ndiye beki bora zaidi wa kulia duniani. Anafahamika zaidi kwa
shughuli yake uwanjani, akipanda kusaidia mashambulizi na kuzuia kwa
ustadi mkubwa. 9
Mtaalamu: Kama Marcelo wa Real, Alves anapanda kushuka
Gerard Pique - Pauni Milioni 5
Katika
kitabu chake binafsi, Sir Alex Ferguson amemtaja beki huyo wa kati
mwenye urefu wa futi 6 na inchi 4 kwamba bora katika kutoa pasi na
anahamasisha ushindi. Anasifika na kuheshimika sana awapo uwanjani
popote. 9
Beki mstaarabu: Pique alisajiliwa tena kutoka Manchester United kwa Pauni Milioni 5
Carles Puyol - Akademi
Akiwa
na umri wa miaka 35 anaweza kuonekana mzee, lakini sentahafu huyo
aliyeichezea mechi 100 Hispania bado ana mengiya kufanya, kwa ujumla
katika mechi za wapinzani hao wa Hispania. Ni mzoefu na anajua kuongoza
vyemka jahazi la timu yake. 8
Mr Barcelona: Ana umri wa miaka 35, lakini uzoefu wa Puyol ni muhimu katika El Clasicos
Adriano - Pauni Milioni 8.1
Adriano - Pauni Milioni 8.1
Akiwa
amepunguziwa mshahara kwa pauni 77, Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka
28 anafahamika kama ‘Utility Man’ na tovuti ya Barca. Beki wa kushoto
chaguo la kwanza aliyefunga mabao mawili msimu huu. 7
Mpiganaji: Beki mwingine anayeshambulia sana, Adriano atakimbiza sana kwenye winga yake leo
Sergio Busquets – Akademi
Ana
kila sababu ya kuitwa mchezaji mkubwa baada ya mafanikio makubwa
aliyoyapata katika mchezo huo. Kiungo huyo tegemeo wa Barcelona ana
Medali za Dhahabu za Kombe la Dunia, Ubingwa wa Ulaya na Kombe la
Ulaya. 9
Mtu wa kazi: Busquets ni kiungo muhimu Barca
Xavi – Akademi
Mtaalamu
wa tiki-taka akiwa na Medali za kutosha bado ni mtu muhimu ndani ya
Barca hususan katika mechi kama hizi. Akiwa na umri wa miaka 33 bado
anaonekana yuko vizuri na hana dalili za kuchuja hata kesho. 9
Mtu wa kazi: Akili ya Xavi kimchezo inamaanisha yeye no bora sana
Andres Iniesta – Akademi
Pacha
huyo wa Xavi katikati ya Uwanja akiwa anazidiwa miaka minne na
mwebnzake huyo, anaweza kuchukua maukumu mara mkongwe huyo
atakapoondoka. Ni mtaalamu wa kutengeneza mabao. 9
Kaka wa kambo: Mtu wa kulia wa Xavi, Iniesta ana muda zaidi wa kucheza Barca
Alexis Sanchez - Pauni Milioni 22
Winga
huyo wa Chile alifahamika duniani baada ya Kombe la Dunia mwaka 2010.
Bado hajafikia haswa ubora ule wa Barca, lakini anaweza kucheza katika
timu hiyo. 8
Winga: Sanchez anahitaji mechi zaidi ili kulata uzoefu na kufikia ubora wa Barca
Neymar - Pauni Milioni 48.6
Hatimaye
ametua Barca msimu huu kuunda safu ya ushambuliaji na mkali mwenzake
kutoka Amerika Kusini, Messi. Akiwa amefunga mabao mawili tu hadi sasa,
atapenda kuweka kumbukumbu zake katika mechi yake ya kwanza wapinzani
hao kucheza. 9
Mchezaji ghali: Neymar amezoea haraka Nou Camp baada ya kununuliwa kwa Pauni Milioni na Barcelona kutoka Santos ya Brazil
Lionel Messi – Akademi
Nini
zaidi unaweza kusema? Hizi ni baadhi ya takwim: Amefunga mabao 18 na
kutoa pasi za mabao 11 katika mechi 25 zilizopita za El Clasicos. Huwa
mtu mwingine kabisa anapocheza dhidi ya Madrid. 10
Hakuna cha kusema zaidi: Messi anapedna kucheza dhidi ya Madrid, na amefunga mabao 18 katika El Clasicos
JUMLA YA GHARAMA: Pauni Milioni 106.7.
VIWANGO KWA UJUMLA: 94/110
VIWANGO KWA UJUMLA: 94/110
Real Madrid (4-2-3-1)
Diego Lopez - Pauni Miloni 3
Alianza
kupewa nafasi na Jose Mourinho badala ya Iker Casillas na Ancelotti
amefuata utaratibu huo. Kipa huyo hodari mwenye urefu wa futi 6 na inchi
5 ni mahiri mno kuokoa michomo. 8/10
Kuelekea mechi: Lopez amempindua gwiji wa Real, Iker Casillas kuwa kipa wa kwanza klabu hiyo
Alvaro Arbeloa - Pauni Milioni 5
Ni
chaguo la kwanza katika beki ya kulia tangu arejee mwaka 2009 katika
klabu hiyo aliyojiunga nayo awali akiwa kinda. Beki huyo wa zamani wa
Liverpool ni nguzo imara katika safu ya ulinzi ya Real. 7
Kisiki: Beki hodari wa kulia aliyeishika beki ya kulia kwa miaka michache iliyopita
Sergio Ramos - Pauni Milioni 23
Beki
asiye na mambo mengi ambaye anatulia na mpira hakika bado ni mtu muhimu
katika klabu hiyo. Katika msimu wake wa tisa Bernabeu ni mtu mwenye
uzito ndani ya chumba cha kubadilishia nguo cha Real. 9
Mtu mzima: Ramos anaunganisha na kuleta umoja ndani ya kikosi, na ana misimu tisa katika klabu hiyo
Raphael Varane - Pauni Milioni 8.5
Beki
wa kati mwenye ufundi wa hali ya juu, alijihakikishia namba kikosi cha
kwanza baada ya kucheza vizuri kwa mara ya kwanza katika Ligi ya
Mabingwa, Real ikiifunga Manchester City msimu uliopita. Akiwa ana umri
wa miaka 20, anaweza kuja kuwa beki wa kati tegemeo wa Madrid miaka
ijayo. 8
Kinda hatari: Akiwa na umri wa miaka 20, Varane (kulia) anaweza kuwa tegemeo la Bernabeu baadaye
Marcelo - Pauni Milioni 5.4
Mbrazil
huyo anashambulia zaidi katika beki ya kushoto, ingawa pia anafanya
vizuri kazi yake ya ulinzi na ana uzoefu sasa wa mechi za wapinzani. 8
Safi: Marcelo anashambulia zaidi
Asier Illarramendi - Pauni Milioni 34
Mchezaji
huyo aliyenunuliwa kwa dau la kiwango cha kati, akiwa ana umri wa miaka
23 ameonyesha ni kiungo hodari mkabaji aliyesajiliwa kutoka Real
Sociedad msimu huu na ameingia kwenye kikosi cha kutokana na Xabi Alonso
kuwa majeruhi, lakini amedhihirisha ubora wake. 8
Presha: lllarramendi aliigharimu Madrid Pauni Milioni 34 kutoka Real Sociedad msimu huu
Sami Khedira - Pauni Milioni 12
Huyu
ni tegemeo la safu ya kiungo ya Madrid. Anaichezesha timu vizuri na
kuvunja mashambulizi ya timu pinzani. Unaweza kumuita kiungo mmoja bora
ambaye anaifanya Real iwe imara. 8
Mashine: Khedira anaiongoza vyema safu ya kiungo ya Real
Gareth Bale - Pauni Milioni 86
Akiwa
amefunga mwanzoni, lakini mchezaji huyo ghali duniani amekuwa na mwanzo
mgumu Real kutokana na kuandamwa na majeruhi yanayomuweka nje ya kikosi
cha timu hiyo kwa muda mrefu. Yuko tayari kucheza El Clasico yake ya
kwanza. 9
Anajipanga: Bale amekuwa na mwanzo mgumu Real, lakini anatarajiwa kucheza leo Nou Camp
Isco - Pauni Milioni 23
Isco - Pauni Milioni 23
Moja
ya sababu za Mesut Ozil kuondoka katika klabu hiyo, Mchezaji huyo namba
10 wa Hispania alikataa ofa ya Manchester City ili kujiunga na timu
hiyo msimu huu. Ameanza na moto akiwa amefunga mabao mabao matano katika
mechi sita. 8
Hiki kifaa: Isco alitakiwa na klabu kadhaa tajiri na kubwa duniani msim huu, lakini akachagua
Cristiano Ronaldo - Pauni Milioni 80
Ameweka
rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao katika mechi sita
mfululizo za El Clasicos. Amefunga mabao 18 katika mechi 14 za klabu na
timu yake ya taifa msimu huu. 10
Mkali kweli: Ronaldo inaelezwa yupo katika kiwango cha juu zaidi maishani mwake katika miaka mitatu iliyopita
Karim Benzema - Pauni Milioni 30
Mshambuliaji
wa kati wa Real asiyepinka kwa sasa baada ya Gonzalo Higuain kuondoka,
lakini akiwa amefunga mabao manne katika mechi 11 msimu huu anaweza
kuanza ili adhihirishe makali yake na kuisaidia timu leo. 8
Mtu wa juu: Benzema (kushoto) sasa ni mchezaji wa kikosi cha kwanza cha Real baada ya kuondoka kwa Higuain msimu uliopita
JUMLA YA GHARAMA: Pauni Milioni 309.9m
VIWANGO KWA UJUMLA: 91/110