Ameenda mbali na kuwatambia wapinzani wao Simba
akiwaeleza wasubiri kipigo Oktoba 20 kwani kikosi cha Jangwani sasa
hakikamatiki.
Cannavaro “Sasa tumeanza, kasi hii ni ushindi
mwanzo mwisho hakuna kusimama. Tumeanza kusogea na sasa tunawakaribia
watani wetu (Simba) kwa karibu kabisa, tunataka tukae wenyewe kileleni.
“Hao Simba wasubiri kipigo tu kwa sababu hawawezi
kutufunga hata kidogo, kama unavyoona kikosi chetu kimekamilika kila
idara kuanzia beki, kiungo hadi ushambuliaji.”
Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 12, tatu
nyuma ya Simba inayoongoza ligi hiyo. Azam FC inashika nafasi ya tatu,
nayo ina pointi 12 pia, lakini imepungukiwa mabao.
Awali Yanga haikuwa na matokeo mazuri katika mechi
zake za nyuma baada ya kufungwa 3-2 na Azam FC na kutoa sare tatu za
bao 1-1 dhidi ya Coastal Union, Mbeya City na Prisons.
Hata hivyo, imeshinda michezo mitatu dhidi ya Mtibwa Sugar (2-0), Ashanti United (5-1) na Ruvu Shooting (1-0).
Kocha Mkuu wa Yanga, Ernest Brandts, kwa upande
wake alisema: “Tunajipanga na kufanya mazoezi kwa bidii kuhakikisha
tunafanya vizuri katika kila mechi iliyopo mbele yetu, nia ni kutetea
ubingwa wetu.”